Posts

Showing posts from May, 2017

MAN U KUPAMBANA BILA NYOTA WAKE ALHAMISI HII

Image
Hofu imetanda kwa mashabiki wa klabu ya Machester United ya nchini Uingereza kuelekea katika mchezo wao wa Nusu fainali ya Europa League ambao utakaofanyika siku ya Alhamisi. United katika mchezo wake wa kwanza wa nusu fainali, huenda ikawakosa wachezaji wake Nyota wa kikosi cha kwanza cha Mreno Jose Mario dos Santos Mourinho, wachezaji hao wakiwa ni pamoja na Bailly , Chris Smalling paomoja na Phil Jones. Wengine ambao wapo katika hati hati ya kukosekana ni Zlatan Ibrahimovic, Marcos Rojo na Timothy Fosu-Mensah Mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa, Paul Pogba anatarajiwa kurejea katika mchezo huo, utakaofanyika nchini Hispania baada ya kukosa mechi mbili kutokana na kuwa majeruhi.

REAL MADRID vs ATLETICO MADRID SHOO YA KIBABE UEFA

Image
Hatua ya nusu fainali ya kwanza katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya (UEFA), inatarajiwa kuanza kuchezwa usiku wa leo (Jumanne). Mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi duniani ni ule wa Real Madrid watakao wakaribisha Atletico Madrid katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu. Hii ni mara ya tano kwa timu hizi kukutana katika michuano ya kombe hili, ambapo mara ya mwisho walikutana misimu miwili iliyopita katika hatua ya fainali ambapo Real walinyakua kombe hilo kwa jumla ya penalty 5-3, baada ya kutoka sare ya 1-1 katika dakika 120. Mechi nyingine ya nusu fainali ya kombe hilo itawakutanisha FC Monaco dhidi ya Juventus Jumatono katika uwanja wa Stade Lois II uliopo mjini Monaco. Mechi nyingine za marudiano zinatarajiwa kuchezwa Mei 9 na 10 ya wiki ijayo.

HIMID MAO ATIMKIA RANDERS FC YA BARNI ULAYA

Image
Mchezaji wa klabu ya Azam FC na Taifa Stars, Kiungo Himid Mao amekwea pipa jana jioni akielekea nchini Denmark, kwa ajili ya majaribio ya kutafuta kucheza soka la kulipwa katika bara la Ulaya. Kiungo huyo machachari anakwenda kufanya majaribio yake ya soka la kulipwa katika klabu ya Randers FC ambayo iko katika ligi kuu nchini Denmark maarufu kwa jina la Superliga. Mao amekuwa katika kiwango cha juu katika ligi ya msimu huu pamoja na michuano mingine ambayo kiungo huyo amekua akicheza. Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amethibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo akisema, “Tuna wachezaji zaidi ya sita wameenda ulaya kwa majaribio, na Mao ni mmoja wao. Taarifa zingine tutatoa kama klabu ila Mao ana baraka zote za klabu kuondoka.  Amepata nafasi ya kuondoka, na hakuna atakaemzuia, wote wataondoka na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu wote tunaamini watafanikiwa na wataweza kuanza maisha mapya katika nchi moja wapo.”