Posts

Showing posts from November, 2017

CHELSEA YAPATA PIGO

Image
Michael Emenalo alikuwa moja ya wakurugenzi wa masuala ya ufundi ndani ya klabu ya Chelsea ambaye pamoja na uwezo wake lakini anaijua vyema Chelsea kwani amekaa klabuni hapo kwa miaka kumi sasa. Tangu Emenalo awe katika bodi ya ufundi ya Chelsea wamefanikiwa kushinda makombe ya Epl mara tatu, Europa mara moja na pia wamefanikiwa kombe moja la Champions League katika kipindi chake. Lakini sasa baada ya miaka hiyo 10 hii leo Michael Emenalo ameamua kuachana na klabu ya Chelsea huku habari za ndani zikisema kwamba Michael Emenalo anaelekea kujiunga na klabu ya Monaco. Habari ya Emenalo kuachana na Chelsea inazidi kukuza tetesi ya maelewano mabovu yanayotajwa kuwepo kati ya kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte na baadhi ya viongozi wa klabu ya Chelsea. Habari nyingine toka darajani inasemekana kocha Antonio Conte amejikuta akiingia kwenye ugomvi mpya na beki wa klabu hiyo David Luiz jambo lililopelekea kumuweka nje katika mpambano zidi ya United.

NDEMLA KUMFUATA THOMAS ULIMWENGU SWEEDEN

Image
TAARIFA KWA UMMA Klabu ya Simba inayofuraha kutangaza kuwa mchezaji wake Hamis Said Juma (Ndemla) amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweeden. Ndemla amepata nafasi hiyo katika klabu ya AFC Eskilstuma inayoshiriki ligi kuu, Ndemla anatarajiwa kuondoka nchini kesho ambapo atakuwa kwenye majaribio ya siku 14 nchini humo. Klabu ya Simba inaamini Ndemla atafanya vizurinakufuzu majaribio hayo. Klabu ya Simba inaendelea kuamini katika kutoa nafasi kwa wachezaji wake kwenda nje kujaribu bahazi za kucheza soka la kulipwa.