Posts

Showing posts from March, 2018

MANARA KUACHANA NA CLUB YAKE

Image
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kusema kwa sasa ameamua kuachana na klabu yake ya Manchester United hadi Kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho atakapoondoka. Haji Manara amesema hayo siku moja baada ya klabu yake hiyo kupigwa bao 2 kwa moja na klabu ya Sevilla hivyo Manchester United kuondolewa kwenye mashindano ya klabu bingwa ulaya. "Guys kuna vitu siwezi kuviasi..1.Dini yangu,,2.wazazi wangu..Mke na watoto wangu na Simba...ila Manchester nimeiacha hadi Mourinho aondoke...Europe nimebaki na Madrid tu.....Kwangu Jose ndio mtu wa hovyo kupita wote duniani kwa sasa" alisema Haji Manara Siku tatu zilizopita wakati Manchester United ikikipiga na Liverpool aliahidi kama timu yake itafungwa angehama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia CHAUMA lakini baahati nzuri timu yake ikashinda ila baada ya kupigwa na Sevilla ameamua kukaa pembeni mpaka kocha Jose Mourinho atakapoondoka.

WAMBURA AWEKWA KIKAANGONI TFF

Image
Kamati ya maadili ya TFF imekutana leo Machi 14, 2018 pamoja na mambo mengine kujadili suala la Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Michael Wambura, aliyefikishwa kwenye kamati kwa makosa matatu.  Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, amesema kuwa kosa la kwanza analokabiliwa nalo Wambura ni kupokea fedha za TFF. Pili, malipo yasiyo halali na tatu ni kugushi  barua na kushusha hadhi ya TFF.