VIWANDA VYA KOROSHO KUJENGWA NCHINI

SERIKALI imo katika mchakato wa kuanzisha kiwanda cha korosho Mkuranga, Mtwara na Tunduru katika mwendelezo wa juhudi za kuwa na Tanzania ya uchumi wa kati na ya viwanda. Tanzania inazalisha tani 260,000 za korosho kwa mwaka na sasa ina viwanda 12 vya ubanguaji. Akizungumza Dar es Salaam jana juu ya umuhimu wa kuacha utaratibu wa kusafirisha korosho ghafi zinazoyanufaisha mataifa mengine, Mtafiti Kiongozi wa Programu ya Korosho Barani Afrika ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Profesa Peter Masawe, amesema kiasi kikubwa cha thamani ya korosho kinapotea kwa kukosa umakini. “Wabanguaji wa Tanzania wanachukua korosho karanga tu huku wakiacha kiasi kikubwa cha zao hilo ikiwemo maganda na mabibo ambayo yana thamani kubwa. Tutafute namna ya kuyaongezea thamani maganda na mabibo badala ya kutupa,” alisema. Profesa Masawe alitolea mfano mataifa yanayonufaika na korosho za Tanzania ikiwemo India: “Tujiulize kwa nini mataifa ya India, China na Vietnam ndio walionunu...