MAN U KUIVURUGA ENGLAND

Manchester United wanajiandaa kutoa ofa ya kunasa saini ya winga wa Chelsea, Willian na beki wa Tottenham Toby Alderweireld, kwa mujibu wa taarifa kutoka ESPN.
Jose Mourinho bado ni shabiki mkubwa wa Willian tangu walipokuwa wote pale Stamford Bridge ambapo Mbrazil huyo hajafurahishwa na kitendo cha kuwekwa benchi mara kwa mara na Antonio Conte msimu huu.

Alderweireld, bado hajakubaliana na Spurs kuhusu mkataba mpya wa kubaki London na klabu yake inatarajiwa kumuuza ili kutunisha mfuko wa usajili majira ya kiangazi.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU