Posts

Showing posts from February, 2017

SERENGETI BOYS YAFUZU FAINALI ZA AFRIKA NCHINI GABON

Image
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ hatimaye imefuzu kushiriki fainali za Afrika zitakazofanyika nchini Gabon, Aprili mwaka huu. Serengeti imefuzu baada ya kushinda rufaa waliiyomkatia mchezaji wa Congo Brazzaville, Langa-Lesse Bercy anayedaiwa kuwa na umri mkubwa aliyetakiwa kwenda kupimwa vipimo maalum cha kuthibitisha umri halisi. Taarifa zilizopatikana jana Ijumaa jioni kutoka mkutano wa CAF nchini Gabon zilidai Serengeti ilipewa nafasi hiyo na sasa itakuwa kati ya timu 8 zitakazocheza fainali hizo. Waziri wa Michezo, Nape Nnauye ameipongeza timu hiyo katika ujumbe wake kupitia akaunti yake ya Twitter. “Mungu Mkubwa! Tumefuzu kwenda fainali za Afrika Chini ya Umri wa miaka 17. NIA, UWEZO NA SABABU ZA KUCHUKUA KOMBE HILI TUNAZO. HONGERA TZ!,” alitweet waziri huyo.

ATLETICO MADRID YAKUBALI KICHAPO

Image
Barcelona wameifunga Atletico Madrid katika mzunguko wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Copa del Rey katika dimba la Vicente Calderon. Katika mchezo huo ulioisha kwa Atletico Madrid kuchapwa 2-1 huku magoli ya Barcelona yakifungwa na Messi pamoja na Suarez na lile la Atletico likipachikwa na Griezman, ilishuhudiwa Messi akifikisha magoli 200 katika michezo 274 ya ugenini. Mchezo wa marudiano utakuwa Februari 7 ambapo Barcelona itakuwa katika dimba lake la nyumbani Camp Nou. Alaves na Celta Vigo ni timu nyingine ambazo zitacheza nusu fainali Februari 8.

DONALD TRUMP AMKATIA SIMU WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA

Image
Mawasiliano ya simu kati ya Rais wa Marekania Donald Trump na waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull, yamezua maswali kuhusu makubaliano ya kuwachukua wakimbizi. Gazeti la Washington Post liliripoti kuwa bwana Trump alitaja mawasiliano hayo kuwa mabaya zaidi kati ya yale aliyoyafanya na viongozi wa dunia siku hiyo, ambapo aliikata simu hiyo. Bwana Trump kisha aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa atafanyaia uchunguzi makubaliano hayo. Makubaliano hayo yaliyoafikiwa wakati wa utawala wa Rais Obama, yatasababisha hadi watafuta hifadhi 1,250 wanaoelekea Australia kupewa hifadhi nchini Marekani. Australia imekataa kuwakubali wakimbizi wengi wao wakiwa ni wanaume kutoka Iran, Afghanistan na Iraq na badala yake wamewazuilia katika vituo vilivyvo kwenye visiwa vya Nauru na Papua New Guinea. Waziri mkuu Turnbull amekuwa akitaka kujua hatma ya makubaliano hayo baada ya Trump kusaini amri ya kuzuiwa kwa muda wakimbizi kutoka nchi saba zilizo na waislamu wengi kuingia nchini Mare...

KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI DRC ETIENNE TSHISEKEDI AFARIKI DUNIA

Image
Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, amefariki dunia mjini Brussels nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 84. Tshisekedi alikwenda mjini Brussels mwishoni mwa mwezi jana kwa ajili ya matibabu. DR Congo: Tshisekedi asafirishwa Ubelgiji kwa matibabu Tshisekedi: Tutamuonyesha 'kadi nyekundu' rais Kabila Utata DRC; wapinzani wadai ratiba ya uchaguzi wa mwaka huu Watu 20 wauawa katika maandamano DR Congo Bwana Tshisekedi alikuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe waliokuwa mstari wa mbele kupigania demokrasia ya nchi yake. Alisimama kidete katika utawala wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Rais Mobutu Sese Seko, ambae utawala wake ulidumu kwa miongo kadhaa kabla ya kupinduliwa. Etienne Tshisekedi pia alikuwa mpinzani wa Rais Laurent Kabila, ambae aliingia madarakani mnamo mwaka 1997, na mwanae, Rais Joseph Kabila, ambae hivi sasa ndio anatawala nchi hiyo.

PAUL MAKONDA JINO KWA JINO NA WAUZA UNGA DAR

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataja askari 9 wanaotuhumiwa kushirikiana na wafanya biashara ya madawa ya kulevya. Aidha amewataja wasanii wanaojihusisha na matumizi na uuzaji wa Madawa ya kulevya na kuwataka kuripoti kituo cha polisi kesho. Akiongea na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake Alhamisi hii, RC Makonda amewataka wauzaji wote kufika makao makuu ya polisi kwajili ya kujieleza. “Nimeamua kuingia kwenye hii vita kwa sababu najua siku moja Mungu ataniuliza, nilikupa mkoa wa Dar es salaam kupitia Rais John Pombe Magufuli watoto waliangamia kwa Madawa ya kulevya, sitaki kufika mbungini nisiwe na jibu, nipo tayari kupoteza ukuu wangu wa mkoa, nipo tayari kutangulia kwa aliyeniumba lakini niwe na jibu kwa mungu wangu aliyeniumba kwamba Madawa ya kulevya hayakubaliki ndani ya Dar es salaam,” alisema Makonda. Aliongeza,’Wapo tuliowakamata pamoja na dawa zao tumeshawafikisha Central Polisi na wanaendelea na mambo yanayotakiwa. Lakini wapo ambao bado, majina...

TAZAMA AGIZO LA RAIS MAGUFULI LILIVYOTEKELEZWA KWA VITENDO.

Image

SAKHO ATUA CRYSTAL PALACE KWA MKOPO

Image
Klabu ya Crystal Palace ambayo inashiriki ligi kuu ya Uiengereza imekamilisha usajili wa beki Mamadou Sakho kutoka klabu ya Liverpool. Mamadou Sakho amejiunga na Crystal Palace kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu akitokea Liverpool.