ZANZIBAR RASMI MWANACHAMA KAMILI WA CAF
Hatimaye mkutano mkuu wa 39 wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) unaoendelea mjini Addis-Ababa, Ethiopia, umepitisha ombi la chama cha soka Zanzibar (ZFA) kuwa mwanachama rasmi wa CAF. Ni jambo la kihistoria kwa Zanzibar kwani safari hii ombi lao limepitishwa bila kupingwa na inakuwa nchi ya 55 mwanachama wa kujitemea wa CAF. Awali Zanzibar ilikuwa inaunganishwa na Tanzania bara chini ya TFF na kupelekea kukosa haki za kushiriki kama nchi kwenye mashindano yanayoandaliwa na CAF pamoja na yale ya FIFA. Pendekezo hilo lilipelekwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndugu, Jamal Malinzi na lilipokelewa na wajumbe 54 wengine waliokuwepo. Hii maana yake ni kuwa kwa sasa CAF ndio shirikisho mwanachama wa FIFA kwa upande wa mabara lenye wanachama wengi zaidi kuliko wote. Vilabu vya Zanzibar vimekuwa vikishiriki mashindano mbalimbali ya CAF lakini kwa ngazi ya kitaifa hawakuwa na ruhusa na walicheza kwa kuungana na Tanzania bara na kushiriki kama Tanzania. Kwa maana ...