HAYATOU APIGWA BAO NA AHMD AHMAD URAIS CAF

Tokeo la picha la ahmad ahmad madagascarRais wa chama cha soka cha Madagascar Ahmad Ahmad ameushtua ulimwengu wa soka baada ya kumbwaga Issa Hayatou ambaye alikuwa rais wa muda mrefu wa shirikisho la soka Barani Afrika na kushinda urais wa Caf.
Uchaguzi uliomalizika Addis Ababa umempa ushindi Ahmad Ahmad baada ya kupata kura 34 dhidi ya 20 za Issa Hayatou.
Matokeo hayo yanahitimisha miaka 29 ya utawala wa Hayatou kama kiongozi wa juu wa soka la Afrika.Mipango na mbinu kabla ya uchaguzi zimepelea kuwashangaza wengi baada ya kushuhudia kambi ya Hayatou ikidondoshwa.
Hayatou mwenye miaka 70 sasa, alikuwa rais wa CAF tangu mwaka 1988 wakati huo Lionel Messi akiwa na miezi tisa tu tangu azaliwe wakati mtawala huyo mzaliwa wa Cameroon alipotangazwa kusimamia soka la bara la Afrika.
Alianza kutawala tangu March 10, 1988 alikuwa anaifukuzia rekodi ya kuendelea kusalia madarakani kwa awamu ya nane mfululizo.Uchaguzi ulifanyika leo baada ya mkutano mkuu wa 39 huko mjini Addis Ababa.Ahmad anakuwa rais wa saba wa CAF kwenye historia ya shirikisho hilo lenye miaka 60 hadi sasa tangu kuanzishwa kwakwe.
Aliingia madarakani akiwa rais wa chama cha soka cha Madagascar mwaka 2003 na sasa amefanikiwa kuwa rais wa CAF kwa miaka minne ya kwanza, ameahidi kuboresha shirikisho hilo na kuwa la kisasa ili kuendana na wakati huku akisema atahakikisha kunakuwa na uwazi wa hali ya juu.
Hayatou aliwahi kupata upinzani mkubwa mara mbili kabla ya sasa lakini mara zote alishinda kwa kishindo, lakini safari hii ameishia kupata kura 20 ambazo zimemaliza matumaini yake ya kutawala kwa zaidi ya miongo mitatu.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU