MKUDE, AJIB WASAINI KANDARASI MPYA SIMBA SC



Tokeo la picha la jonas mkude

Na Hussein Mkuwia

Mwenyekiti wa usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe unaweza ukasema amecheza kama Pele mara baada ya kukamilisha mipango ya usajili kwa Ibrahim Ajib na Jonas Mkude wachezaji waliokuwa wanaelekea mwisho mwa mikataba yao. 

Wawili hao mikataba yao ilikuwa inaisha mwishoni mwa msimu huu lakini wamekubali kuongeza mikataba ya miaka miwili kila mmoja.

Kwenye mikataba yote ya wachezaji hao, kila mchezaji anaruhusiwa kwenda kufanya majaribio kwenye klabu itakayoomba mchezaji husika kufanya hivyo na kuhama kama taratibu zitafuatwa.

Hii Ni Habari nzuri kwa wapenzi wa klabu ya Simba kwani wachezaji hao ni nguzo kubwa klabuni hapo kwasasa.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU