MANCHESTER UNITED YAPATA PIGO

Manchester United huenda ikapata pigo kubwa zaidi kwa mchezaji wake Zlatan Ibrahimovic ambaye ameonekana kuwa tegemeo katika ufungaji magoli ndani ya timu hiyo.



Kwa mujibu wa ESPN imeripoti kuwa kuna uwezekano mchezaji huyo asionekane uwanjani tena mpaka Januari mwakani, kutokana na majereha aliyoyapata usiku wa Alhamisi katika mechi ya ligi ya Europa, waliyocheza dhidi ya Anderlecht.

Katika mechi hiyo, Ibrahimovic alitolewa nje na kushindwa kuendelea na mchezo huo katika dakika ya 90, baada ya kuumia mguu wake wa kulia alipotua chini baada ya kuruka juu.
Mkataba wa mchezaji huyo na Man United unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu huku timu ya LA Galaxy inayocheza ligi kuu ya Marekani, ikionekana kutamani kumsajili mchezaji huyo.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU