CHADEMA YAZADI KUWA KIVUTIO CHA MAWAZIRI

Baada ya Mhe.Lazaro Nyarandu kuachana na CCM na kuomba kujiunga na Chadema,nimejaribu kukumbuka idadi ya mawaziri wakuu,mawaziri,manaibu waziri ambao wamehamia Chadema,kwa haraka nimepata idadi ipatayo nane akiwemo Lowassa,Sumaye,Kingunge,Ntagazwa,Makongoro,Lau Masha,Ole Medeye(baadaye alihamia UDP) na sasa Nyalandu. Hawa wote walipata kuongoza Wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti. Pia mhe.Ruth Mollel huyu alikuwa Katibu Mkuu wa wizara na sasa yupo Chadema. Kwa hali ilivyo je idadi inweza kuongezeka? Maana wapo wanaomtaja Mhe. Nape kuwa yupo mbioni kuhama na wengine pia. Zipo habari kuwa Chadema wamekuwa wakipita pita na kujigamba kuwa watawachukua wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama hasa wakitajwa viongozi wawili wa TISS, Apson Mwangonda na Hassy Kitine kuwa ni watu wao.