OKWI AIREJESHA SIMBA SC KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA

Ligi kuu soka Tanzania Bara iliendelea tena hapo jana lakini macho na maskio ya wadau na wapenzi wasoka yalikuwa yameelekezwa huko katika Uwanja wa Uhuru ambapo mabingwa wa FA, Simba SC wakiwa wenyeji waliwakaribisha Mtibwa Sugar.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa nakasi na vuta nikuvute baina ya timu zote mbili wenyeji wa mchezo huo Simba walikubali kuruhusu bao la mapema katika kipindi cha kwanza dakika ya 37 likifungwa na nahodha wa Mtibwa Sugar, Stamili Mbonde kwa njia ya kichwa.
Hadi dakika 90 za mchezo Mtibwa Sugar ilikuwa ikiongoza hali iliyopelekea hadi baadhi ya mashabiki wa Simba kukata tamaa na kuanza kuondoka Uwanjani.
Katika dakika tatu za nyongeza mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda na klabu ya Simba, Emmanuel Arnold Okwi akaendeleza ufalme wake wa mabao baada ya kufunga goli lake la saba kwenye uwanja huo wa Uhuru na kuinusuru timu yake kupoteza kwa mara ya kwanza mechi ya ligi kuu msimu huu.
Bao safi la Emmanuel Okwi lilipatikana baada ya kupiga faulo iliyokwenda moja kwa moja nyavuni ikiwa ni adhabu iliyotolewa na muamuzi baada ya mchezaji wa Simba "Erasto Nyoni" kufanyiwa rafu karibu na eneo la penati.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo Emmanuel Okwi amesema “Mtibwa ni timu kubwa na nzuri tulikuwa tumesha fungwa lakini tunashukuru kwa matokeo haya.” Okwi ameyasema hayo kupitia Azam Tv.
Emmanuel Okwi sasa anafikisha jumla ya mabao saba katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu akiwa ameingia dimbani mara tano wakati akifanikiwa kufunga mabao yote katika michezo ya Dar es salaam na kuiwezesha simba kurejea kileleni ligi kuu.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU