Posts

Showing posts from December, 2017

SINGIDA YAZOA SERENGETI BOYS

Image
Klabu ya Singida United imewekeza kwa vijana baada ya kuwanasa vijana wanne waliokuwa na timu ya taifa ya vijana wa umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys iliyoshiriki michuano ya AFCON 2017 nchini Gabon.  Singida United imeeleza kuwa hatua hiyo nni mipango ya klabu katika kusaidia vijana wenye vipaji na vimeshaonekana katika ngazi ya taifa.  Pamoja na hilo usajili huo umeelezwa kuwa ni mipango ya maboresho ya kikosi hicho kuwa na timu imara itakayodumu kwa muda mrefu.  Vijana waliosajiliwa ni aliyekuwa nahodha wa Serengeti Boys, Issa Makamba ambaye anacheza nafasi ya kiungo wa kati, mshambuliaji Assad Juma, mlinzi  Ally Ng’azi na mshambuliaji Mohamed Abdallah.  Wachezaji hao wanne wamesaini mkataba wa miaka mitatu kila mmoja na wamelipwa Ada ya usajili (Signing fee) pamoja na stahiki zao zingine ambazo wataendelea kulipwa ikiwemo mishahara.  Katika usajili huu wa dirisha dogo Singida United imeongeza nyota kadhaa ambao ni Daniel Lyanga kutoka Fanj...

RYOBA AWEKA WAZI KILICHOMKUTA LISSU

Image
Mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba Chacha (CHADEMA) amefunguka na kutaja sifa za mtu ambaye alitaka kumuua Tundu Lissu na kusema mtu huyo alishindwa kutekeleza hilo kwa kuwa Mungu hakupanga Lissu aondoke kwa kipindi hicho.  Marwa Ryoba amesema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook baada ya kuweka picha ya Tundu Lissu akiwa hospitali ya Nairobi Kenya na kusema kuwa Mbunge huyo sasa anaendelea vizuri baada ya kutolewa risasi 16 mwilini.  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma, baadaye alisafirishwa na kupelekwa nchini Kenya jijini Nairobi ambapo mpaka sasa anapatiwa matibabu huko.

MBUNGE AWACHANA WANAOHAMA VYAMA

Image
Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema, Upendo Peneza amesema hana sababu za kuhama chama hicho kikuu cha upinzani nchini huku akiwashangaa wanaochukua uamuzi huo.  Aidha mbunge Peneza aliwaomba watanzania kuona namna fedha ya Tanzania inavyochezewa kwa kila siku wabunge na madiwani wakihama kutoka chama kimoja kwenda kingine, hivyo kuliingiza taifa hasara kwa kuandaa chaguzi nyingine.  Huku wale waliohama chama wakipewa nafasi ya kugombea nyazifa, ''kwahiyo ni mchezo mchafu wanaochewa watanzania'' alisema 

NGUVU ZAIPONZA ZANZIBAR HEROES CECAFA

Image
Mawakala wa kupinga utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu Michezoni nchini kupitia tawi lao nchini Kenya (World Anti-Doping Agency “WADA”) kwa kushirikiana na Baraza la Vyama vya Michezo Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) linawasi wasi na  wachezaji wanne wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kutumia dawa hizo. Wachezaji hao ni Kiungo Mohd Issa “Banka”, Fesal Salum “Fei Toto” na Washambuliaji Ibrahim Hamad Hilika na Suleiman Kassim “Seleembe”. Hofu hiyo imekuja kwenye Mashindani ya Cecafa Senior Chalenj Cup jioni ya leo katika uwanja wa Kenyatta Mjini Machakos mara baada ya kutoka sare ya 0-0 na Wenyeji Kenya na kupelekea Zanzibar kutinga moja kwa moja nusu fainali wakiwa na alama 7 wakiongoza kundi lao A lenye Mataifa kama Kenya, Libya, Rwanda na Tanzania bara. WADA na CECAFA wameingiwa na wasi wasi kutokana na kiwango bora walichoonyesha Zanzibar katika Mashindano hayo huku ikiwaongoza mataifa kama Libya, Rwanda, wenyeji Kenya na Tanzania Bara.