NGUVU ZAIPONZA ZANZIBAR HEROES CECAFA



Mawakala wa kupinga utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu Michezoni nchini kupitia tawi lao nchini Kenya (World Anti-Doping Agency “WADA”) kwa kushirikiana na Baraza la Vyama vya Michezo Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) linawasi wasi na  wachezaji wanne wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kutumia dawa hizo.

Wachezaji hao ni Kiungo Mohd Issa “Banka”, Fesal Salum “Fei Toto” na Washambuliaji Ibrahim Hamad Hilika na Suleiman Kassim “Seleembe”.

Hofu hiyo imekuja kwenye Mashindani ya Cecafa Senior Chalenj Cup jioni ya leo katika uwanja wa Kenyatta Mjini Machakos mara baada ya kutoka sare ya 0-0 na Wenyeji Kenya na kupelekea Zanzibar kutinga moja kwa moja nusu fainali wakiwa na alama 7 wakiongoza kundi lao A lenye Mataifa kama Kenya, Libya, Rwanda na Tanzania bara.

WADA na CECAFA wameingiwa na wasi wasi kutokana na kiwango bora walichoonyesha Zanzibar katika Mashindano hayo huku ikiwaongoza mataifa kama Libya, Rwanda, wenyeji Kenya na Tanzania Bara.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU