Posts

Showing posts from August, 2016

WAZIRI WA ELIMU AUWAWA KWA KOSA LA KUSINZIA WAKATI RAIS AKIZUNGUMZA

Image
Serikali ya Korea Kusini imesema waziri wa elimu nchini Korea Kaskazini ameuawa na maafisa wa serikali. Waziri huyo wa elimu anadaiwa kuchunguzwa kwa madai ya kuhusika katika ufisadi baada yake kusinzia katika mkutano wa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un. Tangazo la kifo cha Kim Yong-jin limetolewa na wizara ya muungano ya Seoul na limetolewa siku chache baada ya taarifa za gazeti moja kusema maafisa wawili wakuu wa Korea Kaskazini waliuawa kwa kulipuliwa kwa makombora ya kutungua ndege. Gazeti hilo lilisema wawili hao waliuawa mapema mwezi huu. Mapema mwezi huu, naobu balozi wa Korea Kaskazini nchini Uingereza aliikimbia nchi yake na kuhamia rasmi Kusini .

MBOWE AVUNJA UKUTA

Image
# Habari :Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mh.Freeman Mbowe amesitisha shughuli za maandamano zilizokuwa zimepewa jina la (UKUTA) kwa Muda  wa mwezi mmoja baada ya kuombwa na viongozi wa Dini na taasisi Mbalimbali, ambapo maandamano hayo yalitarajiwa kufanyika Septemba mosi nchi nzima.

SERIKALI KUTANGAZA AJIRA ELFU 71 MWAKA HUU WA FEDHA

Image
Serikali imewatoa hofu wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kuwa itaanza zoezi la kuajiri punde tu itakapokalimisha zoezi la uhakiki watumishi hewa nchini. Waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, Angela Kairuki amesema hayo kwenye kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ kinachorushwa na TBC 1 ambapo amebainisha kuwa jumla ya ajira elfu 71 zinatarajiwa kutangazwa katika kipindi cha mwaka huu wa fedha. “Ukiangalia katika mwaka huu wa fedha ajira ambazo tunatarajia kuzitoa katika serikali ni takribani elfu 71 na 496 hatujafuta ajira hizo ni lini tu mchakato huo unaanza ndicho ambacho tumekuwa tumekiahirisha kwa muda mfupi na nipende kuwatia moyo kuwa waendelee kusubiri wasijiinge katika makundi ambayo hawastahili kuingizwa waendelee kuwa na uadilifu na muda si mrefu wataingia katika utumishi wa umma”, alisema Kairuki. Akizungumzia suala la watumishi hewa, Waziri Kairuki alisema serikali imebaini watumishi 16,127 baada ya kufanya zoezi la kuhakiki katika idara ...

CUF YAWASIMAMISHA UANACHAMA PROFESA LIPUMBA, SAKAYA NA LUGEYE

Image
Chama Cha Wananchi (CUF) kimewasimamisha uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Bara, Magdalena Sakaya.   Uamuzi huo umetolewa jana na Baraza Kuu la Chama hicho lililofanya mkutano wake visiwani Zanzibar kwa lengo la kuwajadili wanachama kadhaa wakiwemo vigogo hao. Sakaya amevuliwa nyadhifa zote ndani ya chama kabla ya kusimamishwa.   Taarifa kutoka ndani ya Mkutano huo zimeeleza kuwa Baraza hilo limewaadhibu wanachama 15 wakiwemo Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua. Mbali na vigogo hao, wengine waliopigwa rungu na Baraza Kuu la CUF ni pamoja na Katibu wa Baraza la Wazee, Shashi Lugeye, Thomas Malima na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano, Abdul Kambaya.   Aidha, Baraza hilo limemsimamisha uanachama Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma. Hatua hii inaweka matatani ubunge wa Sakaya na Nachuma kwani wakifikia hatua ya kufukuzwa watakosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.   ...

WAZIRI NAPE AVIFUNGIA VITUO VYA RADIO

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo  Nape Nnauye ametangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni  Magic Fm  ya Dar es salaam na  Radio 5  ya Arusha kwa makosa ya kutangaza na kutoa habari za kichochezi. ‘ Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza August 29 2016 hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake, kimsingi radio zote mbili kwa pamoja wametangaza na kutoa habari ambazo zina uchochezi ndani yake ‘ – Waziri Nape Nnauye

WAZIRI NAPE AVIFUNGIA VITUO VYA RADIO

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo  Nape Nnauye ametangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni  Magic Fm  ya Dar es salaam na  Radio 5  ya Arusha kwa makosa ya kutangaza na kutoa habari za kichochezi. ‘ Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza August 29 2016 hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake, kimsingi radio zote mbili kwa pamoja wametangaza na kutoa habari ambazo zina uchochezi ndani yake ‘ – Waziri Nape Nnauye

KOCHA NIGERIA ABWAGA MANYANGA

Image
Samson Siasia kocha mwenye mafanikio makubwa kwenye soka la Afrika kwenye michuano ya Olympics akiwa amewahi kutwaa medali ya fedha Beijing mwaka 2008, amelalamika kwamba hajalipwa na waajari wake (Nigeria Football Federation (NFF) kwa muda mrefu sasa. Siasia Amesema, ameachana na soka la Nigeria baada ya kupambana kwenye michuano ya Olympics iliyomalizika nchini Brazil. “Nimefikia ponti ambapo naweza kusema sasa inatosha hapa nilipofikia,” Siasia ambaye mkataba wake umemalizika baada ya michuano ya Olympics aliiambia BBC Sports. “Nimekuwa silipwi kwa miezi kadhaa, miaka mingi nimekuwa siheshimiwi na mamlaka ya soka Nigeria lakini sasa imetosha.” “Licha ya kutwaa medali ya shaba kwenye michuano ya Olympics nchini Bralzil lakini wachezaji, makocha na maafisa wote wa timu hawajapokea pongezi zozote wala asante,” aliongeza Siasia.

HENRY SHAVU ULAYA

Image
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal ambaye pia alikuwa akifanya kazi kama mchambuzi wa masuala ya soka kwenye kituo cha televisheni cha Skysports ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa nchi ya Ubelgiji chini ya Roberto Martinez. Henry hivyo ataenda kutengeneza jopo la makocha pamoja na Graeme Jones, ambaye alikuwa msaidizi wa Martinez kule Swansea, Wigan na Everton. Henry alisema “najsikia mwenye furaha kubwa na ninajisikia vyema kuchaguliwa kushika nafasi hii. Namshukuru Roberto Martinez na pia chama cha soka cha nchini Ubelgiji. Nina furaha sana, na sitaki kungoja”. Martinez alisema “Thierryni mtu wa muhimu sana na ataleta kitu kikubwa na cha msingi sana kwenye kikosi chetu. Ni vyema sana kuwa nae”. “Henry ni mtu anayejua kutengeneza akili sahihi na muono unaotakiwa kwa wachezaji, namna ya kufanya kazi pamoja na kushinda. Alitwaa ubingwa wa dunia mwaka 1998 huku pia akiwa na uzoefu wa kushinda mambo mengi.” Henry anategemewa kuongeza uzo...

TFF YAWAFUNGIA WACHEZAJI WALIOSAJILIWA KIJANJAJANJA

Image
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kutoa tahadhali kwa timu tano za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) juu ya kuwatumia wachezaji ambao imewasajili, lakini imebainika mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kwamba wanamatatizo kwenye usajili wao. Majimaji ya Songea Mchezaji anayefahamika kwa majina ya George Mpole ambaye pia amebainika kuwa ndiye Gerald Mpole wa Majimaji ya Songea amefungiwa kucheza soka kwa mwaka kwa kosa la kubadili jina akiwa na lengo la kufanya udanganyifu kwenye usajili. Majimaji imeagizwa kutomtumia mchezaji huyo kutoka Kimondo FC. African Lyon ya Dar es Salaam Mchezaji Rehani Kibingu aliyesajiliwa na African Lyon ya Dar es Salaam, amesimamishwa kuchezea timu hiyo mpaka uongozi wa African Lyon kumalizana na Ashanti United ya Dar es Salaam kabla ya Agosti 27, 2016. African Lyon isimtumie mchezaji huyo kwa sasa. Mbao FC ya Mwanza Mchezaji Emmanuel Kichiba aliyesajiliwa Mbao FC, naye amesimamishwa mpaka Mbao watakapomali...

MKUU WA WILAYA TUNDURU AKIFUNGIA CHUO

Image
Na Hussein Mkuwia. Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera, akifungia chuo cha VISSION TRAINING GOLLEGE kilichopo wilayani humo. Homera alifanya ziara ya kushitukiza na kujionea hadha wanayokumbananayo wanafunzi wa chuo hicho ikiwemo kutosajiriwa kwa cho hicho katika mamlaka zinazotambulika kisheria na kulala chini ndani madarasa yanayotumika kusomea wakati wa mchana. Hivyo Homera kuagiza chuo hicho kufungwa, kuwarudishia fedha zao wanafunzi hao na kaimu mkuu wa chuo hicho Hassani Muya kukamatwa na jeshi la polisi wilayani hapo.