ZLATAN AZIDI KUWA MTAMU UNITED

Zlatan Ibrahimovic amefunga mabao mawili akiicheza kwa mara ya kwanza kwenye dimba la Old Trafford kama mchezaji wa Manchester United na kuzidi kuisogeza timu hiyo kileleni zaidi.1
Mkali huyo wa magoli alifunga goli la kwanza baada ya kupokea krosi maridhawa iliyochongwa kutoka upande wa kulia na Wayne Rooney.
Zlatan alifunga bao la pili kwa njia ya penati baada ya beki wa kushoto wa Man United Luke Shaw kufanyiwa madhambi na Jordy Clasie.
Paul Pogba, ambaye amesajili kwa paundi mil 89 kutoka Juventus kwa mara ya kwanza jana
ameichezea klabu hiyo na kuonesha uwezo mkubwa sana.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU