Posts

Showing posts from August, 2017

RONALDO NDANI KIKOSI CHA MADRID DHIDI YA MAN UNITED UEFA SUPER CUP

Image

SNEIJDER AMFUATA MARIO BALOTELLI UFARANSA

Image
KIUNGO nyota wa Kidachi, Wesley Sneijder ameungana tena na staa mwenzake wa zamani klabuni Inter Milan,Mario Balotelli baada ya jioni ya leo kujiunga na klabu ya OGC Nice ya nchini Ufaransa. Sneijder mwenye umri wa miaka 33 amejiunga na OGC Nice kwa mkataba wa mwaka mmoja ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu atupiwe virago na klabu yake ya zamani ya Galatasaray aliyoichezea kwa kipindi cha miaka minne iliyopita. Kiungo huyo aliyewahi kutamba na vilabu vya Ajax pamoja na Real Madrid amepewa jezi namba 10 ambayo hapo awali ilikuwa ikivaliwa na Mickael Le Bihan. Hii ni mara ya pili kwa Sneijder na Balotelli kucheza klabu moja.Awali ilikiwa ni mwaka 2010 ambapo wawili hao waliichezea Inter Milan na kufanikiwa kutwaa taji la michuano ya kombe la klabu bingwa Ulaya chini ya kocha Jose Mourinho.

SINGIDA UNITED YANASA MTAMBO WA MAGOLI KUTOKA KAIZER CHIEFS NA MANYIKA JR NAYE NDANI

Image
Singida United wamefunga usajili kwa staili ya aina yake baada ya jana usiku kumsajili straika wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Mzimbabwe Michelle Katsavairo. Katsavairo mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Singida United kwa mkopo wa msimu mmoja hii ni baada ya kushindwa kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Kaizer Chiefs. Kabla ya kutua Kaizer Chiefs,Katsavairo aliwahi kutamba na vilabu vya nyumbani kwao Zimbabwe vya Platinum FC pamoja na Chicken Inn F.C. Mbali ya Katsavairo mwingine aliyenaswa na Singida United ni mlinda mlango Peter Manyika Jr aliyekuwa akiidakia Simba sc. Manyika amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mkataba wake na Simba kuishia,wakati huohuo Singida United imemtoa kwa mkopo wa msimu mmoja kwenda Stand United nyota wake Mzimbabwe,Wisdom Mutasa.

KAULI YA NIYONZIMA BAADA YA KUTAMBULISHWA MSIMBAZI

Image
KIUNGO mpya wa klabu ya Simba, Haruna Kizimana Niyonzima(Fabregas) ametambulishwa rasmi na klabu ya Simba ikiwa ni siku moja tu tangu atue jijini Dar es Salaam akitokea nchini kwao Rwanda. Niyonzima ambaye amejiunga na Simba akitokea kwa watani wa jadi wa Simba (Yanga) alitambulishwa rasmi kwenye mkutano na wana habari uliofanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Msimbazi jijini Dar es Salaam ambapo pia alipata fursa ya kuongea kwa mara ya kwanza akiwa kama mchezaji wa Simba. “Kwasasa mimi ni mchezaji halali wa Simba na mambo mengine ni uwanjani” alisema Niyonzima huku akishangiliwa na kundi kubwa la wanachama wa klabu hiyo waliokuwa wamejitokeza kwenye mkutano huo. Simba wamefanya utambulisho huo mbele ya waandishi wa habari ambapo waliwakilishwa na Haji Manara ambaye ni msemaji Mkuu wa klabu ya Simba, Kocha msaidizi wa kikosi cha Simba, Jackson Mayanja, nahodha mpya wa klabu hiyo,Method Mwanjale, Mchezaji bora wa kikosi cha Simba kwa msimu uliopita,Mohamed Hussein ...