SNEIJDER AMFUATA MARIO BALOTELLI UFARANSA
KIUNGO nyota wa Kidachi, Wesley Sneijder ameungana tena na staa mwenzake wa zamani klabuni Inter Milan,Mario Balotelli baada ya jioni ya leo kujiunga na klabu ya OGC Nice ya nchini Ufaransa.
Sneijder mwenye umri wa miaka 33 amejiunga na OGC Nice kwa mkataba wa mwaka mmoja ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu atupiwe virago na klabu yake ya zamani ya Galatasaray aliyoichezea kwa kipindi cha miaka minne iliyopita.
Kiungo huyo aliyewahi kutamba na vilabu vya Ajax pamoja na Real Madrid amepewa jezi namba 10 ambayo hapo awali ilikuwa ikivaliwa na Mickael Le Bihan.
Hii ni mara ya pili kwa Sneijder na Balotelli kucheza klabu moja.Awali ilikiwa ni mwaka 2010 ambapo wawili hao waliichezea Inter Milan na kufanikiwa kutwaa taji la michuano ya kombe la klabu bingwa Ulaya chini ya kocha Jose Mourinho.
Comments
Post a Comment