SINGIDA UNITED YANASA MTAMBO WA MAGOLI KUTOKA KAIZER CHIEFS NA MANYIKA JR NAYE NDANI

Singida United wamefunga usajili kwa staili ya aina yake baada ya jana usiku kumsajili straika wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Mzimbabwe Michelle Katsavairo.
Katsavairo mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Singida United kwa mkopo wa msimu mmoja hii ni baada ya kushindwa kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Kaizer Chiefs.

Kabla ya kutua Kaizer Chiefs,Katsavairo aliwahi kutamba na vilabu vya nyumbani kwao Zimbabwe vya Platinum FC pamoja na Chicken Inn F.C.

Mbali ya Katsavairo mwingine aliyenaswa na Singida United ni mlinda mlango Peter Manyika Jr aliyekuwa akiidakia Simba sc.

Manyika amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mkataba wake na Simba kuishia,wakati huohuo Singida United imemtoa kwa mkopo wa msimu mmoja kwenda Stand United nyota wake Mzimbabwe,Wisdom Mutasa.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU