KAULI YA NIYONZIMA BAADA YA KUTAMBULISHWA MSIMBAZI
KIUNGO mpya wa klabu ya Simba, Haruna Kizimana Niyonzima(Fabregas) ametambulishwa rasmi na klabu ya Simba ikiwa ni siku moja tu tangu atue jijini Dar es Salaam akitokea nchini kwao Rwanda.

“Kwasasa mimi ni mchezaji halali wa Simba na mambo mengine ni uwanjani” alisema Niyonzima huku akishangiliwa na kundi kubwa la wanachama wa klabu hiyo waliokuwa wamejitokeza kwenye mkutano huo.
Simba wamefanya utambulisho huo mbele ya waandishi wa habari ambapo waliwakilishwa na Haji Manara ambaye ni msemaji Mkuu wa klabu ya Simba, Kocha msaidizi wa kikosi cha Simba, Jackson Mayanja, nahodha mpya wa klabu hiyo,Method Mwanjale, Mchezaji bora wa kikosi cha Simba kwa msimu uliopita,Mohamed Hussein ‘Tshabalala’pamoja na wachezaji wapya wa klabu hiyo ambao ni Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima na Nicholaus Gyan.
Comments
Post a Comment