Posts

Showing posts from January, 2017

TAZAMA SEDIO MANE ALIVYOSHINDWA KUIVUSHA SENEGAL ROBO FINAL AFCON 2017 ...

Image

CODE

NONDO DRIVE: keys : BC54C53E1DFDADCF1FCB41A829FF950E05black

RAIS MAGUFULI AAGIZA MAGALI BINAFSI YATAKAYOPITA BARABARA ZA MWENDOKASI YANG'OLEWE MATAIRI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameviagiza vikosi vya Usalama Barabarani kuwashughulikia wanaoingiza magari kwenye njia za mwendokasi kwani wanavunja sheria za nchi. Rais huyo ameyasema hayo Jumatano hii jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa magari hayo, eneo la Gerezani, Kariakoo huku akiagiza watakaokiuka wakamatwe na kupelekwa vituo vya polisi ama kung’oa matairi kwenye magari yao ili liwe fundisho kwao na kwa wengine. “Trafiki mkiona pikipiki, gari linatumia barabara hizi za mwendokasi yashikeni pelekeni kituo cha polisi, yatoeni matairi ili wajifunze. Saa nyingine ukitumia sheria tu watu hawajifunzi lazima mtumie nguvu za ziada ili waziogope hizo barabara za mwendokasi,” amesema Rais Magufuli. Rais Magufuli amezindua rasmi miundo mbinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka (mwendokasi), awamu ya kwanza.

TRUMP ATIMUA WAKENYA 90

Image
Raia takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria. Wote wamewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya. Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameiambia BBC kwamba raia hao wa Somalia watasafirishwa moja kwa moja hadi Mogadishu. “Ni watu 90 kulingana na habari ambazo tulipewa. Wakati unaondolewa nchi fulani kurejeshwa kwenu, huwa unarejeshwa hadi kwenu,” ameambia BBC. Kuhusu sababu iliyowafanya kufurushwa, Bw Kiraithe amesema: “Inategemea sheria za nchi ambayo walikuwa wamehamia (Marekani),” Anatarajiwa kuweka masharti makali kwa raia wa mataifa saba ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye idadi kubwa ya Waislamu wanaotafuta viza za kwenda Marekani. Wakati wa kampeni yake ya urais, Donald Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji Marekani.

ADAMA BARROW AMKUBALIA JAMMEH KUONDOKA NA UTAJIRI WAKE

Image
Rais wa Gambia Adama Barrow anadaiwa alifikia makubaliano na mtangulizi wake, Yahya Jammeh, yanayomruhusu Jammeh kubakia na magari yake ya kifahari ili naye akubali kwenda kuishi uhamishoni Guinea ya Ikweta. Chanzo kimoja kwenye uwanja wa ndege wa Banjul kililiambia shirika la habari la AFP kwamba shehena ya magari ilikuwa ikipakiwa kwenye ndege usiku wa Jumamosi, siku ambayo Jammeh aliondoka nchini Gambia. “Rolls Royce mbili na Mercedes Benz moja ziliingizwa kwenye ndege ya mizigo ya Chad huku magari mengine 10 ya kifahari yakingojea kusafirishwa.” “Serikali ilikuwa imejitayarisha vya kutosha kutoa msaada mkubwa kwa Jammeh aondoke na matokeo yake ikaonekana ni bora aondoke na mali zake zote,” alisema msemaji wa Barrow, Halifa Sallah. Chanzo kilichoko uwanja wa ndege kinasema kuliwahi kuzuka mabishano baina ya serikali na upande wa Jammeh juu ya gari gani ipakiwe kwenye ndege baina ya Bentleys na Rolls Royce, kabla ya baadaye kukubaliana juu ya Rolls Royce. Habari hii huen...

MAFARAO WAONGOZA KUNDI D

Image
Hatua ya makundi ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 maarufu kama  AFCON 2017  imemmalizika kwa usiku wa January 24 kuchezwa michezo miwili ya  Kundi D  ya kukamilisha ratiba ya hatua ya Makundi. Kundi D lilikuwa na timu za  Ghana ,  Mali ,   Misri  na  Uganda  lakini kabla ya michezo ya leo kuchezwa  Misri  na  Ghana  walikuwa tayari wamefuzu kucheza hatua ya robo fainali ila tu mchezo wa leo ulikuwa ni wakukamilisha ratiba na kujua kati ya  Ghana  na  Misri  nani atapata nafasi ya kuongoza  Kundi D . Kwa mara nyingine tena  Mohamed Salah  aliyetoa pasi ya kuiondoa  Uganda  katika michuano ya AFCON 2017, ndio amekuwa hatari kwa  Ghana  baada ya dakika ya 11 kuifunga  Ghana  goli kwa mkwaju wa faulo, goli ambalo lilidumu kwa dakika zote 90 za mchezo 1-0 na kuifanya  Misri  ipate nafasi ya kumaliza kileleni mwa Kundi D...

SUMATRA YAPANGA BEI ELEKEZI YA NAULI KUTOKEA TUNDURU

Image

DIAMOND PLATNUMZ AKIIWAKILISHA TANZANIA- AFCON 2017 ⁄ GABON

Image

WAFUGAJI WAUA MKULIMA

Image
NA HUSSEIN MKUWIA POLISI Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma inawasaka  wafugaji jamii ya Kimang’ati ili kujibu tuhuma ya mauaji ya mkulima katika kijiji cha Lukala tarafa ya Lukumbule.  Katika taarifa hiyo, Kamanda Muhombeji  alimtaja mtu aliyekumbwa na mkasa huo kuwa ni Issa Kasimu Issa  (27) na kwamba mkasa huo ulimpata wakati akiwa katika mazizi ya wafugaji hao nje kidogo ya kijijini hicho. Tukio hilo lilitokea Januari  7, 2017 katika kijiji cha Lukala pembezoni mwa mto Ruvuma,  eneo ambalo walikuwa wakiishi wafugaji hao wanaodaiwa kuwa na urafiki  wa muda mrefu na marehemu, na kwamba walikuwa wakimpatia ng’ombe na kwenda kuwauzia na kuwapelekea fedha.   Hivyo jeshi la polisi mkoani ruvuma limewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zenye usahihi zitakazowezesha watuhumiwa kukamatwa  ili sheria iweze kufuata mkondo wake .

DC TUNDURU AHAIDI KUWASOMESHA WATOTO WANNE

Image
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera(kushoto) akizungumza na watoto alioahidi kuwasomesha   NA HUSSEIN MKUWIA Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mkoani Ruvuma Juma Homera ameahidi kuwasomesha wanafunzi wanne zikiwa ni juhudi za serikali kuhamasisha wazazi kupeleka watoto wao shule hasa awamu hii ambapo serikali ya awamu ya tano inatoa elimu Bure. Waliyopata bahati hiyo adhimu kutoka kwa mkuu wa Wilaya huyo ni wanafunzi waliohaguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari mwaka wa masomo 2017 kutoka katika kijiji cha Nambalapi Kata ya Masonya wilayani humo. Homera alitoa ahadi hiyo wakati akiongea na wananchi wa Kijiji hicho katika mkutano wa kuhamasisha shughuli za maendeleo katika kata hiyo uliofanyika katika viwanja vya ofisi za kijiji hicho. Homera amewataja wanafunzi hao kuwa ni  Somoye Bakari,Awetu Ally,Amina Rajab na Sada Hamisi ambaye ni yatima.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARY 15,2017

Image

AZAMU FC YAMNG'OA MENO MNYAMA NA KUWA BINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI

Image
Wachezaji na Viongozi wa Azam fc wakifurahia ubingwa kombe la mapinduzi katika Uwanja wa Amani. AZAM FC  ndio mabingwa wapya wa michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2017, bada ya usiku huu kuifunga  Simba, bao 1-0, katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Amaan Zanzibar. Kiungo mkabaji Himid Mao Mkami ndiye aliyefunga bao hilo pekee katika dakika ya 13, baada ya kuachia shuti kali la mbali lililomshinda kipa Daniel Angyei wa Simba. Huo unakuwa ubingwa wa nne kwa Azam kuchukua Kombe la Mapinduzi na kuzishinda timu hizo kongwe za Simba na Yanga ambazo zina muda mrefu ukilinganisha na Azam iliyoanzishwa mwaka 2004 na kupanda kucheza ligi ya Vodacom 2008. Katika mchezo huo Simba ndio waliouanza kwa kasi mchezo huo lakini mshambuliai wake Juma Luizi0 akashindwa kumalizia pasi ya Shizza Kichua. Azam walijibu shambulizi hilo dakika ya nane, lakini nahodha wake John Bocco alishindws kuitumia vizuri krosi ya beki wa kulia Gadiel Michael na mpi...

YANGA KUMRUDISHA MKWASA KWENYE BENCHI LA UFUNDI

Image
Klabu ya Yanga inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na kocha wao wa zamani Charles Boniface Mkwasa kwa ajili ya kumrudisha kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo. Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kimeiambia shaffihdauda.co.tz kuwa, kuna uwezekano mkubwa Mkwasa akarejea kwenye benchi la ufundi la Yanga. “Uongozi wa Yanga tayari umeanza mazungumzo na Mkwasa kwa ajili ya kumrudisha kwenye benchi la ufundi baada ya kuachana na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.” Mkwasa ambaye aliondoka Yanga akiwa kocha msaidizi wa Hans van Pluijm kwenda kuifundisha Taifa Stars, baada ya TFF kumfukuza aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mart Nooij. Juma lililopita TFF ilitangaza kuachana na Mkwasa baada ya pande mbili kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba, swali linalobaki ni kwamba, Mkwasa akirudi Yanga ndio mwisho wa Mwambusi?

BEBARTOV AMPA TANO ZLATAN IBRAHIMOVIC

Image
Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya soka ya Manchester United, Dimitar Berbatov amemsifika Zlatan Ibrahimovic na kudai kuwa mchezaji huyo ana uwezo wa kucheza soka kwa miaka miwili zaidi japo umri wake umekuwa mkubwa. Akiongea na Times, Berbatov amesema kuwa japo umri umekuwa kikwazo kwa mshambuliaji huyo lakini amekuwa na uwezo mkubwa wa kufunga magoli lakini pia amemsifia na kiungo wa Everton, Gareth Barry mwenye umri sawa na Ibrahimovic. I don’t think anyone said that [age would be an issue for Ibrahimovic] because he is a player at the top level where the way he plays, he can play for another two years, maybe more. He has that class and understanding of the game and also when to push himself and not waste energy, just the right moment at the right time and he’s there scoring goals,” amesema Berbatov. “He has football intelligence and then of course you have Gareth Barry at Everton. I tend to watch the older players to see how they are playing and I admire both of th...

SCHNEIDERLIN AJIFUNGA KITANZI EVERTON

Image
Morgan Schneiderlin akisaini kandarasi ya miaka minne kuitumika Everton FC Kiungo Morgan Schneiderlin hatimaye amejiunga na klabu ya Everton, akitokea Man United kwa ada ya paundi milioni  20 ambayo itapanda hadi paundi milioni 24. Mfaransa huyo ambaye ana umri wa miaka 27, amesaini mkataba wa miaka minne na nusu ambao utamalizika mwaka 2021, Schneiderlin ameungana na kocha wake wa zamani Ronald Koeman.

PAYET AGOMEA MAZOEZI, ATAKA AUZWE

Image
Kocha wa klabu ya West Ham Slaven Bilic amesema kuwa mshambuliaji Dimitri Payet amekataa tena kuichezea West Ham, lakini klabu hiyo haiko tayari  kumuuza. Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akihusishwa na suala la kuihama timu hiyo. ”Tumesema kuwa hatuwezi kuwauza wachezaji wetu wazuri lakini Payet hataki kutuchezea tena”, alisema Bilic. ”Hatuwezi kumuuza”. Payet alijiunga na West Ham kutoka Merseille kwa kitita cha pauni milioni 10.7 mnamo mwezi Juni 2015. Alifanikiwa katika msimu wa kwanza na klabu hiyo ,akifunga mabao 12 na kuteuliwa miongoni mwa tuzo la wachezaji bora la kila mwaka. Hadi sasa hivi ameshafunga magoli matano katika msimu huu, Payet ameshindwa kufikia kiwango kama hicho na gazeti la The Sun liliripoti wiki ilioipita kwamba Bilic alimuagiza mchezaji huyo kubadili tabia yake. Aliachwa nje katika mechi ya FA siku ya Ijumaa ambapo West Ham ilifungwa 5-0 na Manchester City. West Ham iko nafasi ya 13 katika ligi ya Uingereza, alama sa...