WAFUGAJI WAUA MKULIMA
NA HUSSEIN MKUWIA
POLISI Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma inawasaka wafugaji jamii ya Kimang’ati ili kujibu tuhuma ya mauaji ya mkulima katika kijiji cha Lukala tarafa ya Lukumbule.
Katika taarifa hiyo, Kamanda Muhombeji alimtaja mtu aliyekumbwa na mkasa huo kuwa ni Issa Kasimu Issa (27) na kwamba mkasa huo ulimpata wakati akiwa katika mazizi ya wafugaji hao nje kidogo ya kijijini hicho.
Tukio hilo lilitokea Januari 7, 2017 katika kijiji cha Lukala pembezoni mwa mto Ruvuma, eneo ambalo walikuwa wakiishi wafugaji hao wanaodaiwa kuwa na urafiki wa muda mrefu na marehemu, na kwamba walikuwa wakimpatia ng’ombe na kwenda kuwauzia na kuwapelekea fedha.
Hivyo jeshi la polisi mkoani ruvuma limewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zenye usahihi zitakazowezesha watuhumiwa kukamatwa ili sheria iweze kufuata mkondo wake.
Comments
Post a Comment