AZAMU FC YAMNG'OA MENO MNYAMA NA KUWA BINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI

Azam FC Bingwa Kombe la Mapinduzi
Wachezaji na Viongozi wa Azam fc wakifurahia ubingwa kombe la mapinduzi katika Uwanja wa Amani.


AZAM FC ndio mabingwa wapya wa michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2017, bada ya usiku huu kuifunga Simba, bao 1-0, katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Amaan Zanzibar.

Kiungo mkabaji Himid Mao Mkami ndiye aliyefunga bao hilo pekee katika dakika ya 13, baada ya kuachia shuti kali la mbali lililomshinda kipa Daniel Angyei wa Simba.

Huo unakuwa ubingwa wa nne kwa Azam kuchukua Kombe la Mapinduzi na kuzishinda timu hizo kongwe za Simba na Yanga ambazo zina muda mrefu ukilinganisha na Azam iliyoanzishwa mwaka 2004 na kupanda kucheza ligi ya Vodacom 2008.

Katika mchezo huo Simba ndio waliouanza kwa kasi mchezo huo lakini mshambuliai wake Juma Luizi0 akashindwa kumalizia pasi ya Shizza Kichua.

Azam walijibu shambulizi hilo dakika ya nane, lakini nahodha wake John Bocco alishindws kuitumia vizuri krosi ya beki wa kulia Gadiel Michael na mpira kutoka nje ya lango la Simba.

Dakika ya 13 ndipo Himid Mao, alipofunga bao hilo, baada ya kupokea pasi ya Shomari Kapombe na kupiga shuti kali ambalo lilimshinda kipa Agyei na mpira kujaa wavuni.

Simba waliendelea kupambana kutafuta bao la kusawazisha lakini walinzi wa Azam walikuwa makini kuondosha hatari zote langoni mwao.

Katika dakika ya 38 beki umahiri wa kipa Aishi Manula uliinusuru Azam baada ya kupangua shuti kali la beki Abdi Banda na mpira kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Kocha Joseph Omog, wa Simba aliamua kufanya mabadiliko ya mapema kwa kumtoa kiungo Mwinyi Kazimoto na kumuingiza Laudit Mavugo ambaye pia hakuweza kuisaidia timu hiyo na Azam kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao hilo la Mao.

Kipindi cha pili Azam walikianza kwa kasi na Mao, nusura afunge bao la mapema lakini kipa wa Simba Agyei aliuwahi na kuudaka mpira huo.

Kocha wa Azam Idd Cheche, alifanya mabadiliko kwa kumtoa Josehp Mahundi na Himidi Mao na nafasi zao kuchukuliwa na Frank Domayo na Enock Agyei ambao waliimarisha eneo la kiungo na kuwadhibiti Simba kushindwa kusawazisha bao hilo.

Simba wao waliwatoa Muzamiru Yasini na Shizza Kichuya na kuwaingiza Pastory Athanas na Jamali Mnyate ambao licha ya kupambana lakini walishindw kusawazisha bao hilo.

Simba walijitahidi kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Azam katika dakika ya mwisho lakini alishindwa kuipenya ngome ya ulinzi ya Azam iliyokuwa chini ya Aggrey Moris aliyechaguliwa mchezaji bora wa mchezo huo wa fainali.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU