DC TUNDURU AHAIDI KUWASOMESHA WATOTO WANNE
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera(kushoto) akizungumza na watoto alioahidi kuwasomesha |
NA HUSSEIN MKUWIA
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mkoani Ruvuma Juma Homera ameahidi kuwasomesha wanafunzi wanne zikiwa ni juhudi za serikali kuhamasisha wazazi kupeleka watoto wao shule hasa awamu hii ambapo serikali ya awamu ya tano inatoa elimu Bure.
Waliyopata bahati hiyo adhimu kutoka kwa mkuu wa Wilaya huyo ni wanafunzi waliohaguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari mwaka wa masomo 2017 kutoka katika kijiji cha Nambalapi Kata ya Masonya wilayani humo.
Homera alitoa ahadi hiyo wakati akiongea na wananchi wa Kijiji hicho katika mkutano wa kuhamasisha shughuli za maendeleo katika kata hiyo uliofanyika katika viwanja vya ofisi za kijiji hicho.
Homera amewataja wanafunzi hao kuwa ni Somoye Bakari,Awetu Ally,Amina Rajab na Sada Hamisi ambaye ni yatima.
Comments
Post a Comment