MWANAHALISI WAICHIMBA MKWARA SERIKALI
Wamiliki wa gazeti la mwanahalisi lililofungiwa na serikali wamemtaka Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na michezo Anastazia Wambura kulifungulia gazeti hilo au watakutana mahakamani. Serikali imelifungia gazeti lao kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia Septemba 19 mwaka 2017. Waziri ametakiwa afungulie gazeti hilo ndani ya siku mbili kuanzia Jumatano vinginevyo watamfungulia mashtaka mahakamani. Licha ya kwenda Mahakamani Mwanahalisi itamdai fidia ya Shilingi milioni 41 yeye Naibu waziri binafsi kwa kila chapisho ambalo halitachapishwa kutokana na kufungiwa gazeti hilo. Kauli hiyo imetolewa Jumatano jijini Dar es salaam na mmoja wa wamiliki wa gazeti la Mwanahalisi Saed Kubenea katika mkutano wake na waandishi wa habari. Tayari mwanasheria wao amepeleka barua rasmi Jumanne kwa naibu waziri kwa vile amelifungia gazeti hilo wakati kuna amri ya Mahakama Kuu ya Dar es Salaam ya kutolifungia gazeti hilo. Hatua hii ni kuonyesha jinsi gani magazeti ya Mwanahalisi yanavyo sa...