VINARA wa Ligi Kuu Tanzania bara, Simba wanatarajiwa kuendeleza rekodi yao ya kufanya vizuri bila kupoteza katika mchezo dhidi ya Mbao FC utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Simba inajivunia kwa kila kitu. Inaongoza kileleni kwa pointi 23 katika michezo tisa iliyocheza kati ya hiyo imeshinda saba, imepata sare mbili, ikiwa na jumla ya mabao ya kufunga 17 na kuruhusu kufungwa matatu pekee. Timu hiyo inajivunia mchezaji wake Shizza Kichuya akiongoza katika safu ya ushambuliaji kwa kufunga mabao saba peke yake hadi sasa, huku wengine katika timu nyingine wakifunga kuanzia manne. Hiyo ni kabla ya matokeo ya jana. Iwapo itaendeleza ushindi itajiwekea rekodi ya kucheza michezo 10 bila kupoteza. Lakini pia, macho yataendelea kuwatazama washambuliaji wake wenye uchu wa kufunga wakati wote ambao ni Kichuya, Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo. Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja alisema kuwa ikiwa kikosi chake kitaendeleza umoja ilionao sasa, basi njia itakuwa nyeup...
Bodi ya wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF), imegawanyika vipande viwili kutokana na mgogoro wa uongozi unaoendelea ndani ya chama hicho. Kugawanyika kwa bodi hiyo kumekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wake, Abdallah Katau kutangaza kutomtambua Profesa Lipumba, huku baadhi ya wajumbe wakipinga tamko hilo wakiliita ni batili kwa mujibu wa katiba ya CUF. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wajumbe wenzake, mjumbe wa bodi ya chama hicho, Peter Malebo, alisema hawatambui tamko lililotolewa na mwenyekiti wao kwani bodi hiyo inajiandaa kuwakutanisha mwenyeki wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad ili kuweza kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Alisema kutokana na hali hiyo, watakaa na wajumbe wenzao na kujadili suala hilo kabla ya kuwaita viongozi hao ikiwa ni pamoja na kujadili ushauri wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi. “Tutakaa na...
Comments
Post a Comment