GAZETI LA MWAHALISI LAPIGWA KUFULI

Serikali ya Tanzania imelifungia gazeti la Mwanahalisi kwa miaka miwili zuio hilo pia linahusisha machapisho ya mtandaoni.
Gazeti hilo linafungiwa kwa kile kilicho arifiwa kuwa ni kuchapisha habari za uongo na uchochezi ambazo zinadaiwa kuwa zinaweza kuhatarisha usalama wa taifa.
Mwanahalisi linakuwa gazeti la pili kufungiwa kwa kipindi cha miezi minne .
Gazeti hilo limepigwa kufuli kutokana na kuchapisha mlolongo wa habari ambazo zinasemekana kuwa za kichochezi ikiwemo yenye kichwa cha habari 'Tumwombee Magufuli au Tundu Lissu' iliyochapishwa katika toleo la 409 la tarehe 18-24 Septemba 2017 .
Hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vikimulikwa kwa ukaribu nchini humo. Mapema mwaka huu Raisi Magufuli alionya vyombo vya habari 'visifikiri viko huru kwa kiwango hicho.'

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU