Posts

Showing posts from 2017

SINGIDA YAZOA SERENGETI BOYS

Image
Klabu ya Singida United imewekeza kwa vijana baada ya kuwanasa vijana wanne waliokuwa na timu ya taifa ya vijana wa umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys iliyoshiriki michuano ya AFCON 2017 nchini Gabon.  Singida United imeeleza kuwa hatua hiyo nni mipango ya klabu katika kusaidia vijana wenye vipaji na vimeshaonekana katika ngazi ya taifa.  Pamoja na hilo usajili huo umeelezwa kuwa ni mipango ya maboresho ya kikosi hicho kuwa na timu imara itakayodumu kwa muda mrefu.  Vijana waliosajiliwa ni aliyekuwa nahodha wa Serengeti Boys, Issa Makamba ambaye anacheza nafasi ya kiungo wa kati, mshambuliaji Assad Juma, mlinzi  Ally Ng’azi na mshambuliaji Mohamed Abdallah.  Wachezaji hao wanne wamesaini mkataba wa miaka mitatu kila mmoja na wamelipwa Ada ya usajili (Signing fee) pamoja na stahiki zao zingine ambazo wataendelea kulipwa ikiwemo mishahara.  Katika usajili huu wa dirisha dogo Singida United imeongeza nyota kadhaa ambao ni Daniel Lyanga kutoka Fanj...

RYOBA AWEKA WAZI KILICHOMKUTA LISSU

Image
Mbunge wa Serengeti, Marwa Ryoba Chacha (CHADEMA) amefunguka na kutaja sifa za mtu ambaye alitaka kumuua Tundu Lissu na kusema mtu huyo alishindwa kutekeleza hilo kwa kuwa Mungu hakupanga Lissu aondoke kwa kipindi hicho.  Marwa Ryoba amesema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook baada ya kuweka picha ya Tundu Lissu akiwa hospitali ya Nairobi Kenya na kusema kuwa Mbunge huyo sasa anaendelea vizuri baada ya kutolewa risasi 16 mwilini.  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma, baadaye alisafirishwa na kupelekwa nchini Kenya jijini Nairobi ambapo mpaka sasa anapatiwa matibabu huko.

MBUNGE AWACHANA WANAOHAMA VYAMA

Image
Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema, Upendo Peneza amesema hana sababu za kuhama chama hicho kikuu cha upinzani nchini huku akiwashangaa wanaochukua uamuzi huo.  Aidha mbunge Peneza aliwaomba watanzania kuona namna fedha ya Tanzania inavyochezewa kwa kila siku wabunge na madiwani wakihama kutoka chama kimoja kwenda kingine, hivyo kuliingiza taifa hasara kwa kuandaa chaguzi nyingine.  Huku wale waliohama chama wakipewa nafasi ya kugombea nyazifa, ''kwahiyo ni mchezo mchafu wanaochewa watanzania'' alisema 

NGUVU ZAIPONZA ZANZIBAR HEROES CECAFA

Image
Mawakala wa kupinga utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu Michezoni nchini kupitia tawi lao nchini Kenya (World Anti-Doping Agency “WADA”) kwa kushirikiana na Baraza la Vyama vya Michezo Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) linawasi wasi na  wachezaji wanne wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kutumia dawa hizo. Wachezaji hao ni Kiungo Mohd Issa “Banka”, Fesal Salum “Fei Toto” na Washambuliaji Ibrahim Hamad Hilika na Suleiman Kassim “Seleembe”. Hofu hiyo imekuja kwenye Mashindani ya Cecafa Senior Chalenj Cup jioni ya leo katika uwanja wa Kenyatta Mjini Machakos mara baada ya kutoka sare ya 0-0 na Wenyeji Kenya na kupelekea Zanzibar kutinga moja kwa moja nusu fainali wakiwa na alama 7 wakiongoza kundi lao A lenye Mataifa kama Kenya, Libya, Rwanda na Tanzania bara. WADA na CECAFA wameingiwa na wasi wasi kutokana na kiwango bora walichoonyesha Zanzibar katika Mashindano hayo huku ikiwaongoza mataifa kama Libya, Rwanda, wenyeji Kenya na Tanzania Bara.

CHELSEA YAPATA PIGO

Image
Michael Emenalo alikuwa moja ya wakurugenzi wa masuala ya ufundi ndani ya klabu ya Chelsea ambaye pamoja na uwezo wake lakini anaijua vyema Chelsea kwani amekaa klabuni hapo kwa miaka kumi sasa. Tangu Emenalo awe katika bodi ya ufundi ya Chelsea wamefanikiwa kushinda makombe ya Epl mara tatu, Europa mara moja na pia wamefanikiwa kombe moja la Champions League katika kipindi chake. Lakini sasa baada ya miaka hiyo 10 hii leo Michael Emenalo ameamua kuachana na klabu ya Chelsea huku habari za ndani zikisema kwamba Michael Emenalo anaelekea kujiunga na klabu ya Monaco. Habari ya Emenalo kuachana na Chelsea inazidi kukuza tetesi ya maelewano mabovu yanayotajwa kuwepo kati ya kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte na baadhi ya viongozi wa klabu ya Chelsea. Habari nyingine toka darajani inasemekana kocha Antonio Conte amejikuta akiingia kwenye ugomvi mpya na beki wa klabu hiyo David Luiz jambo lililopelekea kumuweka nje katika mpambano zidi ya United.

NDEMLA KUMFUATA THOMAS ULIMWENGU SWEEDEN

Image
TAARIFA KWA UMMA Klabu ya Simba inayofuraha kutangaza kuwa mchezaji wake Hamis Said Juma (Ndemla) amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweeden. Ndemla amepata nafasi hiyo katika klabu ya AFC Eskilstuma inayoshiriki ligi kuu, Ndemla anatarajiwa kuondoka nchini kesho ambapo atakuwa kwenye majaribio ya siku 14 nchini humo. Klabu ya Simba inaamini Ndemla atafanya vizurinakufuzu majaribio hayo. Klabu ya Simba inaendelea kuamini katika kutoa nafasi kwa wachezaji wake kwenda nje kujaribu bahazi za kucheza soka la kulipwa.

CHADEMA YAZADI KUWA KIVUTIO CHA MAWAZIRI

Image
Baada ya Mhe.Lazaro Nyarandu kuachana na CCM na kuomba kujiunga na Chadema,nimejaribu kukumbuka idadi ya mawaziri wakuu,mawaziri,manaibu waziri ambao wamehamia Chadema,kwa haraka nimepata idadi ipatayo nane akiwemo Lowassa,Sumaye,Kingunge,Ntagazwa,Makongoro,Lau Masha,Ole Medeye(baadaye alihamia UDP) na sasa Nyalandu. Hawa wote walipata kuongoza Wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti. Pia mhe.Ruth Mollel huyu alikuwa Katibu Mkuu wa wizara na sasa yupo Chadema. Kwa hali ilivyo je idadi inweza kuongezeka? Maana wapo wanaomtaja Mhe. Nape kuwa yupo mbioni kuhama na wengine pia. Zipo habari kuwa Chadema wamekuwa wakipita pita na kujigamba kuwa watawachukua wastaafu wa vyombo vya ulinzi na usalama hasa wakitajwa viongozi wawili wa TISS, Apson Mwangonda na Hassy Kitine kuwa ni watu wao.

EZRA CHILOBA AJIONDOA TUME YA UCHAGUZI KENYA(IEBC)

Image
Afisa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi nchini Kenya Ezra Chiloba anatarajiwa kuchukuwa likizo ya wiki tatu na hatoshiriki katika uchaguzi wa marejeo wa Alhamisi kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya. Kulingana na duru katika tume hiyo ya IEBC bwana Chiloba alifanya uamuzi huo wa kibinafsi wa kutoshiriki ili kujenga upya imani ya washikadau ambao wamelalamika kuhusu maafisa wa tume hiyo. Kulingana na gazeti hilo afisa huyo amekuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka muungano wa upinzani Nasa kujiuzulu, huku mgombea wa urais wa muungano huo Raila Odinga akiitisha maandamano ya kumlazimisha kuondoka pamoja na maafisa wengine ikiwatuhumu kwa kusimamia vibaya uchaguzi wa Agosti 8 ambapo rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi. Matokeo ya uchaguzi huo hatahivyo yalifutiliwa mbali na mahakama ya juu ambayo iliamua kwamba haukufanyika kulingana na sheria. Kulingana na Daily Nation Bwana Chiloba anachukua likizo baada ya mwenyekiti wa tume hiyo wafula Chebukati kutaka maafi...

KOCHA WA RAYON SPORTS YA RWANDA NDIYE MRITHI WA MAYANJA SIMBA SC

Image
Klabu ya Simba leo Oktoba 19, 2017 imemtambulisha aliyekuwa kocha wa Rayon Sport ya Rwanda Masoud Djuma kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja ambaye jana ametangaza kuachana na klabu hiyo.  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara mchana wa leo amemtangaza Masoud Djuma kuchukua nafasi ya kocha msaidizi katika klabu yao hiyo ya Simba na kuwaomba wanachama wa mashabiki wa Simba kumpa ushirikiano kocha huyo.  " Tunawaomba wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba mumpe ushirikiano kocha wetu Masoud Djuma yeye ndiye atakuwa msaidizi wa Kocha Omog kuanzia leo Oktoba 19, 2017 na pia tumeboresha benchi la ufundi kwa kumteua meneja mpya Richard Robert yeye anachukua nafasi ya Dkt Kapinga ambaye alikuwa meneja kwa muda tuliokuwa naye mfupi lakini amerudi kwa mwajiri wake nasi klabu tumeona turidhie " alisema Haji Manara.  Mbali na hilo Manara amekanusha taarifa zinazoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kija...

MAYANJA AITOSA SIMBA SC

Image
Kocha Msaidizi wa kikosi cha Simba Jackson Mayanja, leo amefikia uamuzi wa kujiuzulu nafasi yake kutokana na kuitaji muda zaidi wakwenda kushughulikia mambo ya kifamilia. Uongozi wa Simba umemruhusu kuweza kwenda kutatua matatizo ya kifamilia lakini pia imempatia baraka zote na kumtakia kila la kheri katika kazi yake ya kufundisha soka.

OKWI AIREJESHA SIMBA SC KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA

Image
Ligi kuu soka Tanzania Bara iliendelea tena hapo jana lakini macho na maskio ya wadau na wapenzi wasoka yalikuwa yameelekezwa huko katika Uwanja wa Uhuru ambapo mabingwa wa FA, Simba SC wakiwa wenyeji waliwakaribisha Mtibwa Sugar. Katika mchezo huo ambao ulikuwa nakasi na vuta nikuvute baina ya timu zote mbili wenyeji wa mchezo huo Simba walikubali kuruhusu bao la mapema katika kipindi cha kwanza dakika ya 37 likifungwa na nahodha wa Mtibwa Sugar, Stamili Mbonde kwa njia ya kichwa. Hadi dakika 90 za mchezo Mtibwa Sugar ilikuwa ikiongoza hali iliyopelekea hadi baadhi ya mashabiki wa Simba kukata tamaa na kuanza kuondoka Uwanjani. Katika dakika tatu za nyongeza mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda na klabu ya Simba, Emmanuel Arnold Okwi akaendeleza ufalme wake wa mabao baada ya kufunga goli lake la saba kwenye uwanja huo wa Uhuru na kuinusuru timu yake kupoteza kwa mara ya kwanza mechi ya ligi kuu msimu huu. Bao safi la Emmanuel Okwi lilipatikana baada ya kupiga faulo iliyo...

MLIPUKO WAUWA TAKRIBANI WATU 300 SOMALIA

Idadi ya watu waliouawa kwenye mlipuko mkubwa wa bomu katika eneo lenye shughuli nyingi kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumamosi, imefikia watu 300 hadi sasa, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la hahari la Reuters Takriban watu wengine 300 walijeruhiwa kwa mujibu wa AFP, wakati lori lililokuwa limejazwa milipuko lilipolipuka karibu na lango la hoteli. Reuters walimnukuu Ahmed Ali, muuguzi anayefanya kazi kwenye hospitali moja akisema kuwa miili 160 haikuweza kutambuliwa na hivyo ilizikwa na serikali jana. Anasema kuwa miili mingini iliziwa na jamaa zao. Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati zake mwaka 2007. Rais Mohamed Abdullahi "Farmajo" Mohamed alilaumu kundi la al-Shabab kwa shambulizi hilo katili. "Tumethibitisha kuwa watu 300 waliuawa kwenye mipuko huo. Idadi ya waliokufa huenda bado ikaongezeka na kuna watu kadha ambao bado hawajulikani waliko," Abdikadir Abdirahman, mkurugenz...

LADY JAYDEE KUFUNGA NDOA NA SPICY

Image
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Judith Wambula(Lady Jaydee) amesema suala la yeye kufunga ndoa na mpenzi wake Spicy watu waliache kama lilivyo kwani ni ishu ya maisha binafsi zaidi. Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘I Miss You’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa watu kutokuwa na haraka na suala hilo na haelewi ni kwanini amekuwa akiulizwa kila mara. “Kwanini watu wanapenda sana kupangia watu maisha, mgekuwa mnaacha vitu vinaflow , mtu kamaliza shule unanza kumuambia mbona hufanyi kazi wakati mtu labda ameomba kazi hajapata, unaulizwa mara unaolewa lini, unaulizwa unazaa lini waache watu waishi maisha yao, msitengemee vitu sana” amesema Lady Jaydee. “Watu walishakula ubwabwa na mambo yakashindikana vile vile, sasa husilazimishe kama mtu hajajiandaa kwanini mtake kulazimisha ubwabwa?. Wanapenda kumpangia mtu kitu afanye wakati hataenda kuishi naye mwisho wa siku mkumbuke haya ni maisha yangu, kwa hiyo nadhani tungeyaacha tukajikita kwenye muziki tu” a...

"UMALAYA SIO DILI" -GIGGY MONEY

Image
Msanii wa Bongo Fleva na Video Queen, Gigy Money amefunguka kuwa moja ya vitu anavyovichukia katika maisha yake ni umalaya huku akidai tabia hiyo inashusha hadhi ya mwanamke. Gigy Money na Amber Lulu wakiwa kwenye party ya mtoto wa Hamisa Mobetto. Gigy Money amesema anajua kuwa kuna wanawake wanaishi mjini kwa kazi hiyo lakini yeye hawezi kufanya kazi hiyo na ndio kazi anayoichukia maishani mwake. “ Nachukia sana kazi ya umalaya najua watu wengi hasa wasichana wengi wanaifanya na wanaipenda ila haina faida kubwa, faida yake ni ya muda mfupi, “amesema Gigy Money kwenye mahojiano yake na Bongo5 kwenye sherehe ya Mtoto wa Hamisa Mobetto. Hata hivyo, Gigy Money amekiri wazi kuwa alishawahi kudanga kipindi cha nyuma lakini kwa sasa ameacha tabia hiyo.

MKE WA DEO FILIKUNJOMBE ANENA KUHUSU MUMEWE

Ikiwa ni miaka miwili imepita tangu aliyekuwa Mbunge wa Ludewa Deo Haule Filikunjombe afariki dunia, mke wa wake Sarah Habiba amesema Tanzania ina pengo kubwa kwa kumpoteza Deo. Kwenye ukurasa wake wa instagram, Sarah Habiba ameandika ujumbe huo, wakiadhimisha miaka miwili ya kifo chake kwa kufanya ibada takatifu. "Mume wangu leo umefikisha miaka miwili tangu upatwe na mauti, kiukweli umeacha pengo kubwa kwa watanzania, jamii na familia kiujumla, watoto wako wanakumiss sana, mimi mkeo, Mungu akulaze mahala pema peponi mpenzi wangu, ntakukumbuka daima mpenzi", ameandika Sarah Habiba. Deo Filikunjombe alifariki octoba 15, 2015 kwa ajali ya helkopta akitokea Dar es salaam kwenda Ludewa, na kuanguka kwenye msitu wa mbuga ya Selous, akiwa na rubani wake William Silaa ambaye ni baba mzazi wa Jerry Silaa, na msaidizi wa Deo Filikunjombe, Bwana Mkwera. Deo Filikunjombe atakumbukwa kwa uchapa kazi wake na juhudi alizozionyesha kwenye kamati ya Bunge kuibua sakata la Escrow akiwa n...

BUNGE LAFANYA KIKAO NA FAMILIA YA LISSU

Image
Wakati Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiendelea na  matibabu katika Hospitali ya Nairobi , familia yake imefanya kikao cha siri na uongozi ya Bunge kujadili matibabu ya mbunge huyo. Kikao hicho kimefanyika leo Jumatatu jijini Dar es Salaam na imeelezwa kimehudhuriwa na Spika Job Ndugai, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila, Mbunge wa Vunjo, James Mbatia, Mbunge wa Hanang’, Dk Mary Nagu na ndugu watatu wa Lissu, wanaume wawili na mwanamke mmoja. Baada ya kupata taarifa za uwepo wa kikao hicho  Blacknationtz blog  iliweka kambi nje ya Ofisi Ndogo za Bunge tangu saa 3:55 asubuhi na kushuhudia shughuli za kawaida zikiendelea huku kukiwa na watu wachache wanaoingia na kutoka ndani ya ofisi hizo. Ilipofika saa 7:40 mchana, alitoka Mbatia akielekea kwenye gari lake baada ya kumaliza kikao hicho. Mwandishi alimfuata kujua kilichojiri ndani ya kikao hicho, Mbatia alikiri kuwepo kwa kikao hicho lakini hakutaka kuzungumza l...

DIAMOND ASITISHA HUDUMA ZA AFYA AMANA

Image
Mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz amesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo kwa kutembelea hospitali ya Amana ambako amesababisha shughuli zisimame kwa muda. Katika ziara yake hiyo aliyoifanya leo Jumatatu, Diamond ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh4 milioni. Muda wote aliokuwa hospitalini hapo wagonjwa na waliokuwa wakiwahudumia walitoka kwa ajili ya kumuona msanii huyo. Diamond ambaye sasa  anatamba na ngoma yake ya Hallelujah , amesema alifikia uamuzi wa kutembelea kwenye hospitali hiyo kwa kuwa ndipo mahali alipozaliwa. Amesema anajivunia kuwa na watu wazuri wa karibu ambao wanamshauri kurudisha kwenye jamii inayomzunguka. "Najua hospitali kuna mahitaji mengi nikaona kwa uwezo wangu mdogo nami nishiriki kusaidia mahali nilipozaliwa siku ya leo ili nipate pia fursa ya kuwaona watoto waliozaliwa tarehe kama yangu," "Nafahamu kuna changamoto nyingi, niwasihi watu wengine waangalie ni namna gani wanaweza kusaidia," amesem...

MWANAHALISI WAICHIMBA MKWARA SERIKALI

Wamiliki wa gazeti la mwanahalisi lililofungiwa na serikali wamemtaka Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na michezo Anastazia Wambura kulifungulia gazeti hilo au watakutana mahakamani. Serikali imelifungia gazeti lao kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia Septemba 19 mwaka 2017. Waziri ametakiwa afungulie gazeti hilo ndani ya siku mbili kuanzia Jumatano vinginevyo watamfungulia mashtaka mahakamani. Licha ya kwenda Mahakamani Mwanahalisi itamdai fidia ya Shilingi milioni 41 yeye Naibu waziri binafsi kwa kila chapisho ambalo halitachapishwa kutokana na kufungiwa gazeti hilo. Kauli hiyo imetolewa Jumatano jijini Dar es salaam na mmoja wa wamiliki wa gazeti la Mwanahalisi Saed Kubenea katika mkutano wake na waandishi wa habari. Tayari mwanasheria wao amepeleka barua rasmi Jumanne kwa naibu waziri kwa vile amelifungia gazeti hilo wakati kuna amri ya Mahakama Kuu ya Dar es Salaam ya kutolifungia gazeti hilo. Hatua hii ni kuonyesha jinsi gani magazeti ya Mwanahalisi yanavyo sa...

MKUU WA WILAYA TUNDURU AZINDUA UPIGAJI CHAPA NG'OMBE

Image
Katika kutekeleza kwa vitendo sheria ya utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo namba 12 ya mwaka 2010 sambamba na kanuni zake za mwaka 2011 halmashauri ya wilaya ya Tunduru imefanya uzinduzi wa upigaji chapa ng’ombe mapema wiki hii katika Kijiji cha Muhuwesi ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Tunduru Mh.Juma Zuberi Homera. Akisoma taarifa ya uzinduzi wa zoezi hilo la upigaji chapa ng’ombe,Afisa Mifugo na Uvuvi wilaya Dk Frank Mkoma alisema wilaya ya Tunduru ina jumla ya ng’ombe 62,685, mbuzi 5,974, kondoo 3,388 na nguruwe 2,650. Kati ya vijiji 157 vya wilaya ya tunduru ni vijiji 41 vilivyokwisha kufanyiwa matumizi bora ya ardhi na jumla ya hekta 11,480 zimetengwa kwa ajili ya malisho, eneo hili lina uwezo wa kulisha mifugo 11,480. Dk Mkoma alisema Halmashauri kwa awamu ya kwanza wanatarajia kupiga chapa ng’ombe wapatao 62,685 na watapigwa chapa kwenye mguu wa nyuma upande wa kulia. “Katika zoezi hili la upigaji chapa ng’ombe, wafugaji wote wa ngombe waliopo kwe...

UPINZANI KENYA KUFANYA MAANDAMANO KUPINGA TUME HURU YA UCHAGUZI (IEBC)

Image
Chama cha upinzani nchini Kenya NASA kimeitisha maandamano Jumanne nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi IEBC mjini Nairobi. Hatua hii ni ya kushinikiza kujiuzulu kwa baadhi ya maafisa wa juu wa tume hiyo walioshiriki kuandaa uchaguzi mkuu wa August 8 mwaka huu uliobatilishwa na mahakama ya juu nchini. NASA umeeleza kwamba hautovamia makao ya tume ya IEBC kama ilivyotajwa awali kuwatimua kwa lazima maafisa hao, badala yake unasema maandamano yatakuwa ya amani katika barabara za mji mkuu Nairobi kushinikiza kujiuzulu kwao. Hilo ni mojawapo ya masharti iliyotoa NASA kushiriki uchaguzi wa marudio uliotangazwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu. Rais Uhuru Kenyatta ametoa onyo kwa wapinzani ambao amesema watakumbana na mkono wa sheria iwapo maandamano yao yataingilia shughuli za kiuchumi za raia wa nchi hiyo. Im Amesema, 'Endeleeni na maandamano yenu, mukigusa mboga za mama wanaouza barabarani, tuko na nyinyi. Mukigusa maduka ya watu tuko na nyinyi. Lakini kama hamuna lingine...

MAREKANI YAANZA KUIHOFIA KOREA KASKAZINI

Image
Marekani imeilalamikia Korea Kaskazini, kwa kauli yake kuwa ina haki ya kuzitungua ndege za kivita za Marekani hata kama zipo nje ya anga la taifa hilo. Msemaji wa ikulu ya Marekani ya white house Sarah Huckabee Sanders, amewaambia waandishi wa habari kuwa kauli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya kigeni wa Korea Kaskazini kwamba Marekani imetangaza vita,ni ya kipuuzi. Kauli hiyo ya waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini ni kufuatia ujumbe wa Rais Trump kupitia ukurasa wake wa twitter,uliokuwa ukisema utawala wa Pyongyoung hauwezi kudumu kwa muda mrefu. Akizungumza katika kituo cha mafunzo cha kimataifa mjini Washington,Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Kang Kyung-wha, amesema dunia inapaswa kupatiwa nafuu na maudhi ya Korea Kaskazini. "Hakika, hii inaonyesha kuwa Korea kaskazini itaendeleza maudhi yake, na katika mazingira kama haya,sisi Korea Kusini na umoja wa mataifa tunapaswa kulishughulikia suala hili kwa umakini mkubwa,ili kutoendeleza hofu ya madhara y...

TANGAZA BIASHARA YAKO NASI.

Image
TANGAZA BIASHARA YAKO,SHEREHE,MSIBA na SHUGHULI ZAKO ZOZOTE NASI KWA BEI NAFUU. #TUPIGIE +255 753394960 E–mail mkuwiahussein@gmail.com TANGAZA NASI ILI KUWAFIKIA WENGI ZAIDI.                            KARIBUNI SANA.

KENYA YAPOKWA KUANDAA MASHINDANO YA CHAN 2018

Kenya imepokonywa fursa ya kuandaa mashindano ya ubingwa wa Afrika wa mwaka 2018 (CHAN) kufuatia mkutanoa wa kamati kuu ya Caf uliofanyika Accra. Hatua hiyo ilitangazwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari baada ya mkutano wa siku moja uliioongozwa na rais wa Caf Ahmad. Caf inasema uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kuchelewa kwa ripoti za ukaguzi kadha uliofanywa nchini Kenya. Kinyanganyiro hicho ambacho kitashirikisha timu 16 kinatarajiwa kuanza tarehe 12 Januari hadi Februari mwaka 2018. Timu ya ukaguzi ya Caf ilizuru Kenya kuanzia tarehe 11 hadi 17 mwezi huu, na kupata kuwa ni uwanja mmoja tu kati ya viwanja vinne uliokuwa tayari kwa michuano hiyo. Shirikisho la kandanda nchini Kenya (FKF) linasisitiza kuwa lilifanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa mashindano ya CHAN mwaka 2018 yangewezekana kwa Kenya na eneo lote la Afrika Mashariki.

WAZIRI MWAKYEMBE APIGA "STOP" MISS TANZANIA

Image
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amepiga marufuku mashindano ya Miss Tanzania na tuzo za muziki kutokana na ubabaishaji wa waandaaji wa mashindano ya tasnia hizo. Mwakyembe amesema mashindano ya Miss Tanzania yamegubikwa na ubabaishaji kwenye utoaji wa tuzo na kumekuwa na tabia ya kuchelewa kuwapa washindi zawadi wanazoahidiwa jambo linaloleta usumbufu. Waziri huyo ameongeza kuwa watakaotaka kuandaa mashindano hayo ni lazima zawadi wanazoahidi kuwapa washindi zipekwe ofisini kwake. ”Kwa sasa tunanakaa chini na wadau wa burudani juu ya mashindano hayo ila tunataka tuzo ziwe na (guaranteed sustainability) muendelezo wa uhakika na sio kufanyika kwa kubahatisha”, alisema Mwakyembe. Kwa mara ya mwisho mashindano ya za Miss Tanzania yalifanyika mwaka 2016 ambapo ilichukua takribani miezi 6 kwa Kamati ya shindano la Urembo la Miss Tanzania kumpatia mshindi zawadi yake. Gari aina ya (Suzuki Swift) aliloshinda Miss Tanzania 2016 Diana Edward baada ya miezi 6 m...

MWALIMU MBARONI KWA KUMJAZA MIMBA MWANAFUNZI

Image
Mwalimu wa shule ya msingi Samazi iliyoko Wilayani Kalambo mkoani Rukwa, anashikiliwa na polisi wa mkoa huo kwa tuhuma za kumbaka na kisha kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la sita, mwenye umri wa miaka 15.   Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Judith Binyura amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi baada ya mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) kumtaja kwamba ndiye aliyempa ujauzito huo.   "Tumekuwa na utaratibu kuwapima mimba watoto wa shule ili kubaini kama wana ujauzito,  sasa safari hii katika shule ya Samazi imegundulika kuwa mwanafunzi wa darasa la sita amepewa ujauzito na mwalimu wake," amesema .   Mratibu Elimu Kata ya Samazi, Daudi Sengo amesema mwalimu huyo alikuwa akimtuma mwanafunzi huyo kufanya kazi za nyumbani kwake kama kufua, kusafisha nyumba na kumpikia chakula cha jioni na kisha kufanya naye mapenzi mara kwa mara.   Ameongeza awali ilikuwa vigumu kuthibitisha kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi hadi mwanafunzi huyo alipopimwa na kubainika ni mjamzit...

MAAFISA WA TUME YA UCHAGUZI NA MIPAKA KENYA (IEBC) MATATANI

Image
Upinzani nchini Kenya Nasa umempatia mkurugenzi wa mashtaka nchini humo Keriako Tobiko saa 72 kuwafungulia mashtaka maafisa wa IEBC wanaotuhumiwa kuharibu uchaguzi wa Agosti 8. Wakati huohuo upinzani huo umeapa kuwafungulia mashtaka ya kibinafsi maafisa hao wa IEBC. Nasa imesema kuwa mahakama ya juu siku ya Jumatano haikuwaondolea lawama maafisa wa IEBC na kwamba ni sharti washtakiwe kwa kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo. ''Kufuatia uamuzi uliotolewa na mahakama ya juu, afisi yako imesema kwamba inaangazia uamuzi huo kwa kina na kufanya uamuzi wa iwapo itawafungulia mashtaka ya uhalifu maafisa wa IEBC au la.Uelewa wetu ni kwamba makamishna na wafanyikazi wakuu wa IEBC walitekeleza uhalifu'', alisema Mbunge Mathare MP Anthony Olouch. Aliongezea: Kutokana na uchaguzi wa marudio uliotangzwa kufanyika tarehe 26, kctoba 2017, maafisa waliorodheshwa hapa chini hawataruhusiwa kusalia afisini ili kuendeleza uhalifu waliotekeleza. Image caption Mwenyekiti wa tume...