Posts

Showing posts from September, 2016

JARIDA LA FORBES LASIFU NDEGE MPYA ZA MAGUFULI

Image
JARIDA mashuhuri duniani la Forbes, limezitaja ndege aina ya Bombardier Dash8 Q400, ambazo tayari Tanzania imezinunua kuwa ni zenye usalama, zinazotumia mafuta kidogo. Limetabiri kuwa zitakuwa nguzo muhimu kwa usafiri wa bei nafuu kwa nchi mbalimbali . Kwa mujibu wa makala iliyochapishwa na jarida hilo ikiwa na kichwa cha habari “Can Bombardier’s Q400 Save Regional Air Service in the US?”, mwandishi anafafanua faida ya ndege hizo, ikilinganishwa na ndege nyingine zinazofanya usafiri wa ndani nchini Marekani. “Bombadier ina kasi nzuri na ya kutosheleza mahitaji ya safari za ndani kwa kiwango cha kuwa na faida zaidi kibiashara, ikilinganishwa na ndege nyingine za aina yake kama ATR,” linaandika jarida hilo la Forbes. Aidha, jarida hilo linataja faida nyingine ya ndege hizo kuwa ni uwezo wa kutumia mafuta kidogo, jambo litakalosaidia kupunguza gharama za usafiri huo wa ndege nchini kwa wasafiri wa ndani. Jarida hilo linafafanua kuwa kiwango kidogo cha mafuta, kinachotumiwa ...

CUF KUMPA PROF LIPUMBA NAFASI YA KUJIELEZA

Image
KAMATI ya Utendaji ya Taifa ya Chama cha Wananchi (Cuf), imeandaa ajenda ya kumfikisha Profesa Ibrahim Lipumba mbele ya Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho ili ajieleze na kujitetea ni kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kutokana na kitendo chake cha kuvamia ofisi akiwa na wafuasi wake na kusababisha uharibifu wa mali za chama. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Nassor Ahmed Mazrui, kutokana na kitendo cha kuvamia Ofisi Kuu ya chama hicho iliyoko Buguruni, Dar es Salaam na kusababisha uharibifu wa mali, Kamati ya Utendaji ya Taifa imeitisha kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa kitakachofanyika kesho. “Kikao hiki kimeitishwa kwa mujibu wa Ibara ya 85(5) na Ibara ya 108 ya Katiba ya Cuf ya mwaka 1992, toleo la mwaka 2014. Kitafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi kwenye Makao Makuu ya Cuf Zanzibar,” alisema. Alisema kwa mujibu wa Ibara ya 12 (6), (7) na (16) ya Katiba ya Cuf ya mwaka 1992, toleo la mwaka 2014, Kamati ya Utendaji ya Tai...

RONALDO AMKUNJIA SURA ZIDANE

Image
Cristiano Ronaldo ameonesha kitendo cha utovu wa nidhamu mbele ya kocha wake Zinedine Zidane pale alipofanya uamuzi wa kumpumzisha mshindi huyo wa Champions League na European Championship wakati wa game dhidi ya Las Palmas. Ronaldo alikunja sura kuonesha kuchukizwa na maamuzi ya Zidane kuhusu kumpumzisha. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Ronaldo kupumzishwa kwa sababu za kiufundi wakati wa mchezo mgumu. Wakati Ronaldo anapumzishwa dakika ya 72, Real Madrid ilikuwa inaongoza kwa 2-1 mbele ya Las Palmas. Zikiwa zimesalia dakika 5 mechi kumalizika, Las Palmas wakasawazisha kwa goli la Sergio Araujo.

DARAJA LA SALENDA KUANZA KUJENGWA MWAKANI 2017

Image
Serikali imesema ujenzi wa daraja refu kuliko yote nchini la Selander utaanza Juni mwakani.Rais John Magufuli amesema hayo jana baada ya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Song Geum-Young Ikulu jijini Dar es Salaam. Amesema wameshapata fedha kutoka Benki ya Exim ya Korea. Septemba mwaka jana, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisaini hati ya mkataba wa makubaliano ya mkopo wa Dola 91 milioni za Marekani sawa na zaidi ya Sh196 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo. Magufuli amesema mchakato wa kulijenga daraja hilo litakalounganisha eneo la ufukwe wa Coco na Aga Khan kupitia baharini unaendelea vizuri na sasa kampuni inayofanya usanifu kutoka Korea ipo kwenye hatua za mwisho.

JESHI LA SYRIA LATANGAZA KUWEPO KWA MAPIGANO MAPYA MJI WA ALEPPO

Image
Jeshi la Syria limetangaza kuwepo kwa mapigano mapya makali katika harakati za kutaka kurudisha eneo linalodhibitiwa na waasi huko Aleppo, ambako takriban watu laki mbili na nusu wamezingirwa. Jeshi hilo limewataka pia raia kujiepusha kuwa katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi. Limesema njia za kutoka katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi zimewekwa wazi kuruhusu watu kutoka. Tangazo hilo limekuja siku chache baada ya kushambuliwa kwa eneo hilo linalodhibitiwa na waasi, mashariki mwa Allepo. Katika hatua nyingine Marekani na Urusi zimeshindwa kukubaliana jinsi ya kuufufua upya mkataba wa kusitisha mapigano, nchini Syria. Akizungumza baada ya mkutano wao mjini New York, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry amesema Urusi inatakiwa kuonesha umakini wake katika kumaliza ghasia nchini Syria. ''.. Iwapo Urusi itatujia na mapendekezo yenye kujenga tutawasikiliza. Watu wanahitaji kuamini kwa vyovyote vile inastahili kubadilisha mbinu za upi...

MESSI KUKAA NJE YA UWANJA SIKU 21

Image
Usiku wa Septemba 21 Ligi Kuu Hispania iliendelea kama kawaida kwa michezo kadhaa kupigwa, lakini moja kati ya michezo iliyochezwa ni pamoja na mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Atletico Madrid uliomalizika kwa sare ya goli 1-1. FC Barcelona ambao walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani walipata pigo katika mchezo huo ambapo mchezaji wao tegemeo Lionel Messi aliumia mguu wake wa kulia dakika ya 51 na kutolewa nje na nafasi yake kuchuliwa na Arda Turan. Septemba 22 2016 taarifa zimetoka Lionel Messi atakaa nje ya uwanja kwa wiki tatu na atakosa michezo sita dhidi ya Sporting Gijon, Gladbach, Celta Vigo, Deportivo la Coruna na anatazamiwa kuwa fiti katika mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Man City October 19 2016.

NGASSA ASINI KANDARASI YA MIAKA MIWILI OMAN

Image
Mchezaji wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba, Yanga SC, Azam FC na Simba za Dar es Salaam, na kiuongo wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Fanja ya Oman. Ngassa anajiunga na wawakilishi hao wa Oman kwenye Ligi ya Mabingwa ya Asia, baada ya wiki tatu tangu avunje mkataba na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini

KLOPP ALIVUNJA DARAJA LA CHELSEA

Image
Chelsea ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani yakubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa vijana wa Jugen Klopp. Mchezo uliotawaliwa na ufundi wa wachezaji kwa kila idara, hasa katika idara ya kiungo liverpool ilionekana ikitawala mchezo huo kwa muda mwingi na kufanikiwa kujinyakulia ushindi wa magoli 2. Beki wa kati wa Liverpool Dejan Lovren aliifunga goli la kwanza baada ya kuuganisha krosi kutoka kwa Philippe Coutinho kutokana na mabeki wa Chelsea kuchelewa kumkaba. Jordan Henderson, ambaye ni nahodha wa Liverpoo akaongeza la pili baada ya kuachia shuti kali ( thunderbolt) na kwenda mapumziko wakiwa na akiba ya mabao mawili mkononi. Kipindi cha pili Chelsea waliimarika na kupata bao kupitia kwa Diego Costa ambaye aliunganisha pasi ya Nemanja Matic, lakini mpaka mwisho wa mchezo matokeo yalibaki kuwa hivyohivyo. Vijana hao wa Jurgen Klopp pia wameshawaadhibu Arsenal na Mabingwa Watetezi Leicester,jumlisha droo dhidi ya Tottenham, huku wakipoteza mchezo mmoja tu dhidi ya tim...

DK MAGUFULI AFANYA UTEUZA WA WAKURUGENZI NA MAKATIBU TAWALA

Image
Taarifa iliyotolewa leo september 10 2016 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua  Eliya Mtinangi Ntandu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, nafasi ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ilikuwa wazi na uteuzi huu umeanza leo. Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo. Wakurugenzi walioteuliwa  ⦁ Godwin Emmanuel Kunambi – Manispaa ya Dodoma ⦁ Elias R. Ntiruhungwa – Mji wa Tarime ⦁ Mwantumu Dau – Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ⦁ Frank Bahati – Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe ⦁ Hudson Stanley Kamoga – Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ⦁ Mwailwa Smith Pangani – Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ⦁ Godfrey Sanga – Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ⦁ Yusuf Daudi Semuguruka – Halmashauri ya Wilaya ...

MUUAJI WA TAIFA STARS APELEKA KILIO OLD TRAFORD

Image
                                                                                              Iheanacho akifunga goli la pili na la ushindi kwa manchester city ikiwa ugenini. (1-2).

BOSSOU KUKOSA MECHI DHIDI YA NDANDA FC

Image
MIPANGO ya Yanga imetibuka, kwani haitaweza kumtumia beki wake kisiki, Vincent Bossou, ambaye ameng’ang’aniwa nchini kwao, Togo. Yanga kwa muda mrefu imekuwa ikimtumia Bossou ambaye ni nahodha msaidizi kama beki kisiki, lakini mipango hiyo inaonekana kugonga mwamba wiki hii. Juzi Bossou alikuwa na kikao kizito na uongozi wa Taifa lake kilichopelekea kuchelewa kurejea nchini kujiunga na kikosi cha timu ya Yanga ambacho kimeelekea mkoani Mtwara. Yanga imeondoka jana asubuhi kuelekea mkoani humo kwa ajili ya mechi dhidi ya Ndanda FC, mchezo unaochezwa leo katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Bossou aling’ara kwenye kikosi chake mwishoni mwa wiki baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 5-0 walioupata dhidi ya Djibouti kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Gabon. Katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Kegue, mjini Lome, mabao ya The Sparrow Hawks yalifungwa na beki wa Yanga ya Tanzania, Vincent Bossou, Mathieu Dossevi, Fo-Doh Laba na K...

UJUMBE WA KUMTISHIA RAIS DK MAGUFULI WAMPONZA MFANYABIASHARA LEONARD MATERU

Image
Mfanyabiashara Leonard Materu (31) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya kutuma ujumbe wa kumtishia Rais John Magufuli kupitia mtandao wa WhatsApp.Materu ambaye ni mkazi wa Moshi Bar Kwadiwani, alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka yake na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo mbele ya Hakimu Mkazi Magreth Bankika.Akisoma mashitaka Wakili Diana alidai, mshitakiwa huyo amefunguliwa kesi hiyo ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa WhatsApp chini ya Sheria ya Mtandao ya mwaka 2015. Ilidaiwa kuwa, Julai 17, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Materu aliandika ujumbe wenye lengo la kudanganya umma kupitia WhatsApp ukisomeka; “Magu ajiandae tunaenda kupindua mpaka Ikulu.”

TRA YAVUKA LENGO LA UKUSANYAJI KODI KWA MWEZI AGOSTI 2016

Kamishna wa Mamlaka ya mapato nchini TRA amesema, wameweza kukusanya trilion 1.158 kwa mwezi August na hivyo kuvuka lengo la kukusanya trilion 1.152 wakati akiongea na waandishi wa habari. Chanzo: Chanel Ten habari. KATIKA harakati za kuhakikisha kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuongeza wigo wa vyanzo vya Mapato pamoja na kukusanya Mapato kikamilifu. Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo; Kulifanya eneo la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha biashara hapa nchini na kuhakikisha kila mfanyabiashara anakuwa na Mashine ya Kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo. Katika kutekeleza hilo Mawakala wote wa EFDs wamefungua ofisi ya pamoja katika jengo la Al-Falah Towers lililopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo ili kurahisisha upatikanaji wa mashine hizo na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika matumizi ya mashine hizo. Aidha Mkurugenzi wa Huduma na ...

SERIKALI YAIPA MIFUKO YA JAMII MIEZI MITATU KUTEKELEZA UJENZI WA VIWANDA

Image
Serikali imetoa mpaka mwezi wa 12 mwaka huu kwa mifuko ya jamii iwe imefikia hatua ya kutekelezeka ya ujenzi wa viwanda na sio maneno matupu. Naye waziri wa viwanda na biashara Charles Mwijage amesema hakuna mtu ALIYEKURUPUKA kuwapa jukumu la ujenzi wa viwanda mashirika hayo ya hifadhi ya jamii, na asset za mifuko yote ni 1O % mpaka 3O% ya GDP ya nchi. Naye katibu mkuu wa chama cha mashirika hayo amesema viwanda vitajengwa na shirika moja moja na vingine kwa kushirikiana na viwanda vitavyojengwa vitakuwepo vya vipuri na nguo.

KIATU MAALUM CHA PAUL POGBA KUELEKEA MECHI YA MANCHESTER DERBY WEEKEND HII

Image
Kampuni ya vifaa vya michezo ya Ujerumani ADIDAS imetuonyesha kiatu atakachovaa staa wa soka wa Man Utd Paul Pogba kwenye mechi yao na Man City MANCHESTER DERBY   weedend hii. ADIDAS wanadhamini mavazi ya michezo ya Paul Pogba wametengeneza kiatu maalum kwa ajili wa mchezaji wao. Kiatu hichi ni  “Adidas ACE16 + Purecontrol Viper Pack”.          

MOURINHO APATA HOFU KUELEKEA MANCHESTER DERBY

Image
Jose Mourinho anakabiliwa na mtihani mzito kwenye safu yake ya ulinzi kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya mahasimu wao Manchester United wikiendi hii. Kuna uwezekano mkubwa sana Mourinho akaingia uwanjani siku hiyo bila ya mabeki wake wawili wa pembeni kwenye pambano hilo litakalopigwa Old Trafford, ukiwa ni mchezo wa kwanza dhidi ya hasimu wake mkubwa Pep Guardiola. Mourinho ana mashaka makubwa juu ya beki wake wa kushoto Luke Shaw , ambaye alilazimika kusitisha mazoezi kwenye kambi ya England kama tahadhari baada ya kupata maumivu ya nyama za mguu. Kwa upande wa beki wa kulia Antonio Valencia, atachelewa kurudi kutoka kuitumikia timu yake ya taifa Ecuador, ikiwa ni masaa 24 tu kabla ya mchezo huo kufanyika.. Tayari Mourinho atamkosa nyota wake muhimu Henrikh Mkhitaryan, ambaye anauguza majeraha aliyopata wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Romania ilipokuwa ikipambana na Armenia.