DARAJA LA SALENDA KUANZA KUJENGWA MWAKANI 2017
Serikali imesema ujenzi wa daraja refu kuliko yote nchini la Selander utaanza Juni mwakani.Rais John Magufuli amesema hayo jana baada ya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Song Geum-Young Ikulu jijini Dar es Salaam. Amesema wameshapata fedha kutoka Benki ya Exim ya Korea.
Septemba mwaka jana, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisaini hati ya mkataba wa makubaliano ya mkopo wa Dola 91 milioni za Marekani sawa na zaidi ya Sh196 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.
Magufuli amesema mchakato wa kulijenga daraja hilo litakalounganisha eneo la ufukwe wa Coco na Aga Khan kupitia baharini unaendelea vizuri na sasa kampuni inayofanya usanifu kutoka Korea ipo kwenye hatua za mwisho.
Comments
Post a Comment