CUF KUMPA PROF LIPUMBA NAFASI YA KUJIELEZA

Tokeo la picha la LIPUMBA

KAMATI ya Utendaji ya Taifa ya Chama cha Wananchi (Cuf), imeandaa ajenda ya kumfikisha Profesa Ibrahim Lipumba mbele ya Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho ili ajieleze na kujitetea ni kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kutokana na kitendo chake cha kuvamia ofisi akiwa na wafuasi wake na kusababisha uharibifu wa mali za chama.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Nassor Ahmed Mazrui, kutokana na kitendo cha kuvamia Ofisi Kuu ya chama hicho iliyoko Buguruni, Dar es Salaam na kusababisha uharibifu wa mali, Kamati ya Utendaji ya Taifa imeitisha kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa kitakachofanyika kesho.

“Kikao hiki kimeitishwa kwa mujibu wa Ibara ya 85(5) na Ibara ya 108 ya Katiba ya Cuf ya mwaka 1992, toleo la mwaka 2014. Kitafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi kwenye Makao Makuu ya Cuf Zanzibar,” alisema.

Alisema kwa mujibu wa Ibara ya 12 (6), (7) na (16) ya Katiba ya Cuf ya mwaka 1992, toleo la mwaka 2014, Kamati ya Utendaji ya Taifa imeandaa ajenda na kumfikisha Profesa Lipumba mbele ya Baraza hilo ili ajieleze kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa mambo aliyoyafanya.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU