KLOPP ALIVUNJA DARAJA LA CHELSEA


1Chelsea ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani yakubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa vijana wa Jugen Klopp.


Mchezo uliotawaliwa na ufundi wa wachezaji kwa kila idara, hasa katika idara ya kiungo liverpool ilionekana ikitawala mchezo huo kwa muda mwingi na kufanikiwa kujinyakulia ushindi wa magoli 2.

Beki wa kati wa Liverpool Dejan Lovren aliifunga goli la kwanza baada ya kuuganisha krosi kutoka kwa Philippe Coutinho kutokana na mabeki wa Chelsea kuchelewa kumkaba.

Jordan Henderson, ambaye ni nahodha wa Liverpoo akaongeza la pili baada ya kuachia shuti kali ( thunderbolt) na kwenda mapumziko wakiwa na akiba ya mabao mawili mkononi.


Kipindi cha pili Chelsea waliimarika na kupata bao kupitia kwa Diego Costa ambaye aliunganisha pasi ya Nemanja Matic, lakini mpaka mwisho wa mchezo matokeo yalibaki kuwa hivyohivyo.

Vijana hao wa Jurgen Klopp pia wameshawaadhibu Arsenal na Mabingwa Watetezi Leicester,jumlisha droo dhidi ya Tottenham, huku wakipoteza mchezo mmoja tu dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu ya Burnley.

Liverpool wamefikisha alama 10 sambamba na Chelsea na Everton.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU