MOURINHO APATA HOFU KUELEKEA MANCHESTER DERBY
Jose Mourinho anakabiliwa na mtihani mzito kwenye safu yake ya ulinzi kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya mahasimu wao Manchester United wikiendi hii.
Mourinho ana mashaka makubwa juu ya beki wake wa kushoto Luke Shaw , ambaye alilazimika kusitisha mazoezi kwenye kambi ya England kama tahadhari baada ya kupata maumivu ya nyama za mguu.
Kwa upande wa beki wa kulia Antonio Valencia, atachelewa kurudi kutoka kuitumikia timu yake ya taifa Ecuador, ikiwa ni masaa 24 tu kabla ya mchezo huo kufanyika..
Tayari Mourinho atamkosa nyota wake muhimu Henrikh Mkhitaryan, ambaye anauguza majeraha aliyopata wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Romania ilipokuwa ikipambana na Armenia.
Comments
Post a Comment