THOMAS MASHALI AFARIKI DUNIA
Bondia nguli wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali maarufu kama Simba asiyefugika amefariki dunia usiku wa kuamkia leo juma tatu october 31,2016 kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam. Inaelezwa kuwa, Mashali alishambuliwa na watu wasiojulikana na kumuita mwizi, mwili wake uliokotwa vichakani huko maeneo ya Kimara na kufikishwa hospitali ya muhimbili na ndipo umauti ulipomkuta. Taarifa zaidi zitakujia kadiri zitakavyotufikia