STAND FC YAANZA KIBABE HASSAN MUYAO CUP
Mashindano ya kombe la HASSAN MUYAO yameanza kutimua vumbi leo ijumaa october 21,2016 katika kiwanja cha ccm wilayani Tunduru kwa kuzikutanisha Stand FC dhidi ya Chapate FC yenye makao yake mtaa wa Ausilinda.
Mchezo huo ambao ulianza kwa timu zote mbili kushambuliana kwa kasi na zikicheza kwa umakini wa hali ya juu na kutoruhusu kutikiswa chavu za lango la kila timu mpaka kumalizika kwa kipindi cha kwanza Stand FC 0-0 Chapate FC.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na taadhari ya aina yake kwa kila timu, lakini Chapate FC walionekana kuzidiwa na kuruhusu mashambulizi langoni mwao.
Ndipo washambuliaji wa Stand FC wakatumia udhaifu wa safu ya ulinzi ya Chapate FC na kuanza kufungua ukurasa wa magoli dakika ya 55 na 70 yakifungwa na Ballotel, Razack dakika ya 63, huku na Shaibu akafunga ukurasa huo wa magoli dakika ya 82.
Huku goli pekee la kufutia machozi la Chapate FC likiwekwa kimiani na mshambuliaji wa Rashidi dakika za lala kwa buriani 90 na kufanya mbao ya matokeo kusomeka Stand FC 4-1 Chapate FC.
Mashindano hayo yataendelea Jumamosi October 22, 2016 kwa mchezo utakawakutanisha Mgomba FC dhidi ya Red Scorpion(nge wekundu).
Comments
Post a Comment