"YANGA SIO MASUFURIA YA SHUGHULI"

Tokeo la picha la akilimali yahaya
Ikiwa yamesalia masaa machache kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa dharura wa klabu ya Yanga, Katibu wa baraza Wazee wa Yanga Ibrahim Akilimali amesema yeye pamoja na wanachama wengine hawakubaliani na mchakato wa Manji kuikodi klabu ya Yanga.
Akilimali amehoji lilipotoka deni la zidi ya shilingi bilioni 11 kitu ambacho kimewastusha sana wanachama. Wakati huohuo ikaibuka hoja kwamba Mwenyekiti wa klabu hiyo akodishwe Yanga na neno yake kwa miaka 10.
“Yanga ni klabu kubwa sana yenye historia kubwa, haiwezi ikakodishwa sawa na masurufia ya shuhulini”, amesema Mzee Akilimali.
Akilimali amezidi kusema kwamba, Manji angefata utaratibu ili kuwapa nafasi wanachama ya kupatiwa elimu ya faida na hasara ya jambo hilo kabla ya kuwaita wanachama ili wakubali au wakatae mchakato huo kabla ya kutia saini au kutotia saini mkataba huo wa kuthibitisha kukodishwa kwa klabu ya Yanga.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

AZAM FC,SIMBA SC ZAFANYA KUFURU USAJILI DIRISHA DOGO