Popular posts from this blog
ZAMU YA NANI LEO, SIMBA AU YANGA?
HUSSEIN MKUWIA Ligi kuu tanzania bara kuendelea leo katika viwanja tofauti huku michezo inayovuta hisia za mashabiki na wadau wa soka nchini ni mchezo wa Africa Lyon dhidi ya Simba sc na mchezo mwingine ni Tanzania Prison dhidi ya Yanga sc. Ikumbukwe simba sc itakuwa mgeni wa Africa Lyon katika uwanja wa Uhuru jijini Daresalaam huku simba wakipambana kuendelea kulinda kumbkumbu yao ya kutopoteza mchezo wowote ikiwa imecheza michezo 13 hadi sasa. Tanzania prison itakuwa mwenyeji wa Yanga katika uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jijini mbeya,yanga itaingia katika mchezo huo ikwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita wakifungwa goli 2-1 dhidi ya Mbeya city fc ya jijini hapo. Michezo yote itapigwa majira ya saa 10 jioni kwa saa ya Afrika mashariki.
Comments
Post a Comment