MKEMI: "YANGA HAIKODISHWI"

Siku chache baada ya agenda za mkutano mkuu wa dharura wa Yanga kuwekwa hadharani, mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo aliyefutwa uanachama katika mkutano wa dharura uliopita Salum Mkemi amepinga mkutano huo ulioitishwa na Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji ukitarajiwa kufanyika October 23.
Mkemi amesema mkutano huo wa dhrula si halali huku pia akipinga mpango wa timu hiyo kukodishwa kwamba ni kinyume na utaratibu huku akisisitiza kwamba yeye bado ni mwanachama na mjumbe halali wa klabu ya Yanga .
“Mimi bado mjumbe wa kamati ya utendaji, sheria na katiba yangu ndivyo inavyosema, Manji kachaguliwa kama nilivyochaguliwa mimi. Kama vile Magufuli alivyochaguliwa, Rais hawezi kusitisha kazi ya mbunge kwasababu yeye si aliyemchagua. Mbunge amechaguliwa na wananchi, mbunge wa kuteuliwa ndio anaweza akamuondoa, mimi nimepigiwa kura kama Manji alivyopigiwa kura.”
“Huo upuuzi wake anaotaka kuufanya Jumapili utamtokea puani, Yanga wenyewe tupo hatujafa na hatujalala. Yanga haikodishwi, kuna vitu vya kukodisha kama turubai la msiba, sufuria, sinia lakini sio timu ya mpira hivyo vitu hakuna duniani na haitowezekana atafute vitu vingine vya kufanya.”
“Agenda hizo zinatokana na mkutano uliopita ambao ulikuwa batili, kwahiyo hizo agenda na mkutano anaoenda kuufanya ni batili. Chochote kitakachofanyika hakitakuwa na usahihi, mkutano wa dharura agenda yake inakuaga moja tu huwezi kuwa na agenda nyingi kwenye mkutano wa dharura huo ni upuuzi, asitufanye Yanga kama hatuna akili, mkutano mkuu tumeshafanya tarehe June 11 mkutano mkuu kwa mwaka unafanyika mara moja sasa kila siku mkutano mkuu asitufanye sisi wapuuzi.”

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

AZAM FC,SIMBA SC ZAFANYA KUFURU USAJILI DIRISHA DOGO