GENK YA SAMATA YAPAA KILELENI KUNDI F LIGI YA EUROPA
Usiku wa October 20 imepigwa michezo ya UEFA Europa League, lakini kwa upande wa watanzania wao walikuwa wakisubiri kumshuhudia mshambuliaji wao wa kimataifa Mbwana Samatta akiiwakilisha klabu yake ya Genk kwenye michuano hiyo ya Ulaya.
Katika mchezo huo ambao Genk iliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Atletico Bilbao na kukusanya pointi tatu wakiutumia vyema uwanja wao wa nyumbani Cristal Arena, Samatta aliingia dakika ya 56 kipindi cha kuchukua nafasi ya Thomas Buffel.
Magoli ya Genk yamefungwa na Jakub Brabec aliyefungua nyavu za Bilbao dakika tano kabla ya kwenda mapumziko huku zikiwa zimesalia dakika mbili pambano kumalizika, mnigeria Onyinye Wilfred Ndidi akafunga bao la pili na la ushindi kwa Genk.
Genk inaongoza Kundi F ikiwa na pointi 6 baada ya kucheza mechi tatu hadi sasa. Katika mechi zake tatu, imeshinda mbili na kupoteza mechi moja, imefanikiwa kufunga magoli 7 huku yenyewe ikiwa imeruhusu magoli manne hivyo kufanya tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa kuwa magoli matatu.
Comments
Post a Comment