EDDO AIPA SIMBA UBINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA
Mchambuzi wa masuala ya soka nchini Eddo Kumwembe ametoa tathmini yake juu ya mwendelezo mzuri wa matokeo inayopata klabu ya Simba katika mechi zake za ligi kuu Tanzania bara (VPL) tangu kuanza kwa msimu huu ikiwa bado haijapoteza mchezo katika mechi zake 9 ilizocheza hadi sasa.
Eddo amesema ‘Wekundu wa Msimbazi’ wapo kwenye nafasi mzuri ya kutwaa taji la VPL msimu huu baada ya misimu minne mfululizo kupita wakishuhudia taji hilo lienda kwa mahasimu wao Jangwani na kwa matajiri wa dar Azam fc (Chamazi).
“Kwa mtazamo wangu nadhani Simba wapo kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa kwasababu wamesajili wachezaji wazuri. Ukiangalia wachezaji wengi wanaoisaidia Simba kwa sasa ni wachezaji wapya, kwahiyo inaonesha kwamba wamefanya usajili mzuri,” amesema Eddo alipokua akitoa maoni yake kwenye kituo cha radio juu ya mwendelezo mzuri wa matokeo ya klabu ya Simba
“Ukiangalia mlinzi wao wa kulia (Boukungu), Mzamiru, Kichuya, Mwanjale ni wachezaji wapya walioingia kwenye kikosi cha kwanza moja kwa moja na kufanya vizuri tofauti na Simba ya misimu ya karibuni wachezaji wapya walikuwa hawaisaidii sana timu kwahiyo hiki ni kitu kizuri ambacho wamefanya.” Amema Eddo.
Comments
Post a Comment