KICHUYA APA DILI AFRIKA KUSINI

Tokeo la picha la kichuya

Baada ya kuonyesha kiwango cha juu tangu atue klabu ya Simba winga Shiza Kichuya huenda akaihama timu hiyo na kutua Chippa United ya Afrika Kusini baada ya benchi la ufundi la timu hiyo kuvutiwa naye.

Wakala wa kusaka wachezaji wa Chippa, Rodgers Mathaba ameiambia blog ya blacknationtz, kuwa wamevutiwa na mchezaji huyo baada ya kumfatilia katika baadhi ya mechi alizoichezea timu yake ya Simba na anatarajia kutua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo.

“Tumevutiwa na kipaji cha Kichuya na tupo tayari kumnunua endapo tutafikia muafaka na klabu yake anayoichezea ya Simba sc,” amesema Mathaba.

 Hiyo itakuwa ni neema kwa Simba na Kichuya mwenyewe ambaye ametua Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya mkoani morogoro na amekuwa na mwanzo mzuri hadi kufikia hapo alipo.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

AZAM FC,SIMBA SC ZAFANYA KUFURU USAJILI DIRISHA DOGO