KICHUYA FITI KUIKABILI KAGERA SUGAR
WINGA tegemeo wa Simba, Shizza Ramadhani Kichuya yuko fiti kuichezea timu yake leo.
Simba SC leo watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na mfungaji huyo wa bao la kusawazisha dakika za lala salama katika sare ya 1-1 na watani, Yanga Oktoba 1, anaweza kuchezeshwa.
Kichuya aliumia kifundo cha mguu Jumatano Simba SC ikishinda 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City na kuzua hofu ya labda ataukosa mchezo wa leo.
Kichuya yuko fiti kuwavaa Kagera Sugar leo katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara .
“Kichuya anaendelea vizuri na leo (jana) jioni atafanya mazoezi. Kwa upande wangu mimi kama daktari anaweza kucheza, sasa ni uamuzi wa benchi la Ufundi tu kumpanga au akutompanga kesho (leo),”alisema Gembe.
Kichuya Jumatano aliseti bao la kwanza lililofungwa na Ibrahim Hajib kabla ya kufunga la pili Simba SC ikijiimarisha kileleni kwa ushindi wa 2-0.
Comments
Post a Comment