UJENZI WA NYUMBA BUKOBA NI TSH 880 BILIONI
SERIKALI mkoani Kagera imesema tathimini iliyofanyika ya athari za tetemeko la ardhi mkoani hapo imebaini ujenzi wa makazi ya watu kurejea kwenye hali yake kunahitaji Sh bilioni 880 huku ujenzi wa miundombinu ya serikali ukihitaji Sh bilioni tisa.
Mkuu wa Mkoa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, aliyasema wakati akipokea msaada wa fedha na vitu mbalimbali yakiwamo mablanketi na vyandarua kutoka kwa taasisi ya Adra Tanzania ya Kanisa la Adventisti Tanzania lenye makao makuu yake Arusha.
Kijuu alisema hadi sasa fedha zilizoingizwa katika akaunti ya maafa ya Kagera ni Sh bilioni nne ambazo hazitoshelezi katika ujenzi wa makazi ya watu.
Alisema serikali imependekeza vifaa vingine vipelekwe katika taasisi za umma vikiwamo vituo vya afya na shule wananchi waendelee kupata huduma kama ilivyokuwa awali.
Comments
Post a Comment