Posts

Showing posts from November, 2016

RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND

Image
Ratiba: **Saa za Bongo Jumapili Novemba 27 1500 Watford v Stoke City              1715 Arsenal v Bournemouth          1930 Manchester United v West Ham United          1930 Southampton v Everton          Jumamosi Desemba 3 1530 Manchester City v Chelsea       1800 Crystal Palace v Southampton           1800 Stoke City v Burnley               1800 Sunderland v Leicester City               1800 Tottenham Hotspur v Swansea City              1800 West Bromwich Albion v Watford ...

DIOUF AMPONDA STEVEN GERRARD

Image
El Hadji Diouf kwa mara nyingine tena amemkandia mchezaji mwenza wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard baada ya legend huyo kutangaza kustaafu rasmi soka. Muingereza huyu ,36, ambaye alishinda taji la Ligi ya Mabingwa pamoja na matajai ya FA jana ametagaza kustaafu rasmi kucheza soka. Diouf ambaye aliiumikia Liverpool kwa misimu miwili aliwahi kumkosoa Gerrard nyakati za nyuma na kwa mara nyingine tena amerudia kufanya hivyo. "Wakati nilipowasili pale, nilimuonesha kuwa hakuwa chochote," Diouf alisema. "Nilimuuliza,'Ni michuano ipi mikubwa umecheza na watu ni sehemu gani hasa umeacha kumbukumbu kwa watu?' Hakuwa Zinedine Zidane. "Kama mchezaji, namheshimu sana. Ni mchezaji mkubwa. Lakini kama mtu ama binadamu wa kawaida hapana. Nilijitahidi kumfanya afahamu hilo. "Kwangu mimi alikuwa mchezaji wa kawaida kama wengine tu. Alitakiwa ajiweke vizuri na kucheza kama ambavyo alifahamu aliutambua wajibu wake, lakini usiende kwa kocha na kuwachong...

SIKU ZA ANTONY MARTIAL MANCHESTER UNITED ZINAHESABIKA

Image
Jose Morinho amemuonya  Anthony Martial  anayecheza chini ya kuwango kuwa nafasi yake Manchester United inazidi kupotea. Martia aliachwa kwenye kikosi kilichozuru  Feyenoord  katika mechi ya Ligi ya Uropa Alhamisi usiku, ambapo United walishinda 4-0,  Henrikh Mkhitaryan  akishinda kama mbadala wa nafasi ya Mfaransa huyo. Kinda huyo wa miaka 20 akitokea Monaco alijiunga na Manchester United kwa dili ambalo lilidaiwa kufika hadi paundi milioni 58 na kujizolea umaarufu katika goli bomba alilofunga dhidi ya Liverpool katika mechi yake ya kwanza kati ya mabao yake 17 ya msimu uliopita.

"FIDEL CASTRO ALIKUWA DIKTETA KATILI" TRUMP

Image
Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amesema kiongozi wa zamani wa Cuba Fidel Castro alikuwa "dikteta katili" saa chache baada ya Bw Castro kufariki dunia akiwa na miaka 90. Bw Trump amesema: "Leo, ulimwengu umeshuhudia kifo cha dikteta katili aliyewakandamiza watu wake kwa karibu miongo sita. Utawala wake ulikuwa wa watu kuuawa kwa kupigwa risasi, wizi, mateso yasiyoweza kufikirika, umaskini na ukiukaji wa haki za kibinadamu. "Ingawa Cuba inasalia kuwa kisiwa chini ya utawala wa kiimla, matumaini yangu ni kwamba siku ya leo ni mwanzo wa kuondokea mambo ya kuogofya ambayo yamevumiliwa kwa muda mrefu, na kuelekea siku za usoni ambapo watu wazuri wa Cuba hatimaye wataishi kwa uhuru ambao wanastahili sana. "Ingawa mikasa, vigo na uchungu uliosababishwa an Fidel Castro haviwezi kufutwa, utawala wetu utajaribu kadiri uwezavyo kuhakikisha watu wa Cuba hatimaye wanaweza kuanza safari yao ya kuelekea kwa ufanisi na uhuru. Najiunga na Wamarekani wengi kutoka C...

KARELIS AMSUGULISHA BENCHI SAMATTA

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta mambo yanaonekana kuwa si mazuri sana kwa upande wake kadiri siku zinavyokwenda mbele, kwa nini? Uwepo wa Nikolaos Karelis ni kigingi kwa Samatta kupata fursa ya kuonesha uwezo kwake katika timu anayoichezea Ubelgiji KRC Genk . Samatta ametokea benchi kwenye mechi zote alizocheza hadi sasa kuchukua nafasi ya mshambuliaji raia wa ugiriki Karelis Nikolous. Lakini katika mechi waliyoshinda 1-0 dhidi ya Genk Samatta alipewa muda mchache zaidi wa kucheza akiingia dakika ya 85 kuchukua nafasi ya Karelis, dakika chache hizo zilizobaki hazikumtosha Mtanzania huyo kufanya madhara yoyote. Ushindi wa bao 1-0 iliopata KRC Genk dhidi ya Rapid Wien unaipa nafasi timu hiyo inayotumikiwa na Mbwana Samatta kufuzu moja kwa moja hatua ya mtoano ya Ligi ya Uropa msimu huu.

IVO MAPUNDA KUANZISHA KITUO CHA MICHEZO

Image
KITUO cha kuendeleza soka kwa vijana walio chini ya miaka mitano hadi 18 kinatarajiwa kufunguliwa Novemba 26 huko Kitunda Mwanang’ati, Ilala Dar es Salaam. Akizungumza na gazeti hili mmiliki wa kituo hicho golikipa wa zamani wa timu za Simba na Yanga, Ivo Mapunda alisema ameona umuhimu wa kuwafundisha watoto misingi ya soka wangali wadogo. “Kituo kinaitwa Ivo Mapunda Sports Centre, lengo ni kuwafundisha watoto misingi ya soka toka wakiwa wadogo ili kujenga timu ya taifa imara baadae,” alisema Ivo. Pia Ivo ameomba ushirikiano kwa wazazi wote wa Kitunda kwa kuwaruhusu na kuwaleta watoto wao kujifunza soka. Taratibu za kujiunga na kituo hicho zinapatikana siku ya uzinduzi kwa kushirikiana na serikali ya mtaa. Ivo Mapunda ni miongoni mwa wachezaji wa Tanzania ambao wamecheza soka kwa mafanikio makubwa.

RUFANI YA LEMA KUSIKILIZWA JUMATATU

Image
HATIMAYE rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema iliyokatwa na mawakili wake itasikilizwa Jumatatu ijayo. Rufaa hiyo itasikilizwa na Jaji Fatma Masengi ya kuomba mbunge huyo kupewa dhamana baada ya mawakili wanaomtetea jana kusajili maombi ya rufaa namba 112/113 ya mwaka 2016 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ili kudai haki ya dhamana ya Lema aliyonyimwa kutokana na makosa ya kisheria yaliyofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha. Rufaa hiyo imepokewa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na kupangwa kwa Jaji Masengi ambaye ndiye atakayeamua hatma ya Lema kuwa nje kwa dhamana au la. Akizungumza na gazeti hili, mawakili hao ambao ni Sheck Mfinanga na Peter Kibatala walisema tayari wamesajili rufaa yao Mahakama Kuu na wanasubiri siku hiyo ili isikilizwe. Mfinanga alisema wameamua kufungua maombi ya rufaa kwa ajili ya kujua ni kwa nini Lema amekosa dhamana ambayo awali Hakimu Desdery Kamugisha alisema ipo wazi.

SIKUKU YA MAULID KUADHIMISHWA KWA USAFI,KUPANDA MITI NA KUCHANGIA DAMU

Image
WAISLAMU wote nchini wametakiwa kuadhimisha Siku ya Maulid kwa kufanya usafi, kupanda miti na kuchangia damu. Aidha, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Siku ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W). Hata hivyo, ugeni rasmi wa Waziri Mkuu Majaliwa unategemea ratiba yake. Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir wakati akizungumzia Siku ya Maulid ambayo alisema kwa mwaka huu, Maulid itasomwa usiku wa Desemba 11, na kitaifa itafanyika Kata ya Shelui wilayani Iramba Mkoa wa Singida na mapumziko yatakuwa siku inayofuata yaani Desemba 12. Mufti Zubeir alisema Waislamu wanatakiwa kutumia siku hiyo kuonesha matendo mema na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu pamoja na kuisaidia jamii kufanya usafi kwenye mitaa yao na kuchangia damu ili kusaidia wenye uhitaji huo. Alisema anatakiwa kiongozi kufanya matendo hayo wanapoifurahia siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambaye amesema uislamu ni usafi, basi...

MAJALIWA AWANG'AKIA WAAJIRI WANAONYANYASA WAFANYAKAZI

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haitawavumilia waajiri ambao hawatoi mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao na amewaonya waache tabia hiyo mara moja Ametoa agizo hilo jana (Jumatano, Novemba 23, 2016) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere ulioko Chuo cha Mipango, nje kidogo ya mji wa Dodoma. Akijibu hoja ya waajiri kutokutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi ambayo iliibuliwa kwenye risala yao, Waziri Mkuu alisema kifungu cha 14 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004  kinaelekeza aina mbalimbali za mikataba inayotakiwa kutumika kuajiri wafanyakazi.  “Kisheria mwajiri anao wajibu wa kuhakikisha kila mtumishi wake ana mkataba wa kazi kwa maandishi,” alisisitiza. Akijibu hoja kuhusu wafanyakazi kuwekwa ndani kiholela, kunyanyaswa, kushushwa vyeo na kusimamishwa kazi na wanasiasa, Waziri Mkuu alisema Serikali chini ya uongozi wa Dk...

SOMA HABARI ZILIZOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 24, 2016

Image

SIMBA SC KUGOMEA MICHEZO DHIDI YA WATANI WAO WA JADI YANGA SC

Image
Uongozi wa klabu ya Simba umesema hautacheza mchezo wowote wa ligi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga endapo waamuzi hawatotoka nje ya nchi tena wenye uzoefu wa mechi kubwa wanaotambuliwa na FIFA. Simba wako tayari kulipa gharama za waamuzi hao kuanzia mwamuzi wa kati na wasaidizi wake wawili ili haki itendeke kwakua watani wao wamekuwa wakipendelewa mara kwa mara na marefarii wa hapa nchini. Msimamo huo umetolewa na msemaji wa klabu hiyo Haji Manara alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari klabuni hapo na kusema kuwa kwa sasa hawatakuwa tayari kuona haki zao zikidhulumiwa kwa namna yoyote na wataanzia mzunguko wa pili unaotarajiwa kuanza Disemba 17. "Simba haitacheza mechi yoyote dhidi ya Yanga ikichezeshwa na waamuzi wa nyumbani, tupo tayari kulipa gharama zote za kuwaleta marefarii kutoka nje ya nchi ili kuepuka hujuma za watani wetu. "Kila mtu aliona jinsi mwamuzi Jonensia Rukyaa alivyotunyonga msimu uliopita na Martin Saanya mechi iliyopita sasa h...

GARETH BALE KUKOSA MCHEZO WA EL CLASICO DISEMBA 3. 2016

Image
Bosi wa Real Madrid Zinedine Zidane amekiri kwamba Gareth Bale anaweza kuukosa mchezo wa El Clasico baada ya kuumia jana katika mchezo dhidi ya Sporting Lisbon. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales alitolewa nje baada ya kuumia kifundo cha mguu katika kipindi cha pili kwenye mchezo huo nafasi yake kuchukuliwa na Marco Asensio. Ukubwa wa jeraha bado haujathibitishwa, lakini Zidane amebainisha kwamba Bale anaweza kuwa bado hayupo fiti kuelekea mchezo huo utakaofanyika Desemba 3. Akiongea na waandishi baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sporting, Zidane alisema: "Bale ameumia kifundo cha mguu lakini anahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi kesho (leo) ili kuona ukubwa wa tatizo. "Ni mapema mno kusema ni muda gani atakuwa nje au ukubwa wa tatizo linalomkabili. Tunasubiri ripoti ya wataalam, hatujui kama atakuwa fiti kwenye mchezo wa El Clasico." Kwa sasa Real wapo kileleni mwa La Liga wakiwa na alama nne zaidi ya Mabingwa Watetezi Barca, wakati huo hu...

RATIBA YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA LEO JUMATANO 23 NOVEMBA. 2016

Image

ABDI BANDA KUTIMKA MSIMBAZI

Image
Ujumbe ambao unaenea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu post ya mchezaji kiraka wa Simba Abdi Banda ambaye inaonesha amepost ujumbe kwenye account yake ya Instagram unaoashiria safari yake imefikia ukingoni ndani ya ‘Wekundu wa Msimbazi.’ “Umefika wakati wa kuwaaga nashukuru kwa upendo wenu mlionionesha. ‘Bahati haikuwa mbali na hali ninapotoka’ SABC, VPL,KFL, otea nadondokea wapi?,” huo ni ujume unaosomeka kwenye account ya Instagram ya Banda inayojulikana kwa jina la abdbandafans. Banda amekuwa hapati nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha kwanza cha Simba tangu kuanza kwa msimu huu chini ya kocha Joseph Omog, msimu uliopita Banda aliwahi kupisha na kocha msaidizi wa klabu hiyo Jackson Mayanja alipomwambia akafanye warm up wakati wa mchezo dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.