IVO MAPUNDA KUANZISHA KITUO CHA MICHEZO
KITUO cha kuendeleza soka kwa vijana walio chini ya miaka mitano hadi 18 kinatarajiwa kufunguliwa Novemba 26 huko Kitunda Mwanang’ati, Ilala Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili mmiliki wa kituo hicho golikipa wa zamani wa timu za Simba na Yanga, Ivo Mapunda alisema ameona umuhimu wa kuwafundisha watoto misingi ya soka wangali wadogo.
“Kituo kinaitwa Ivo Mapunda Sports Centre, lengo ni kuwafundisha watoto misingi ya soka toka wakiwa wadogo ili kujenga timu ya taifa imara baadae,” alisema Ivo.
Pia Ivo ameomba ushirikiano kwa wazazi wote wa Kitunda kwa kuwaruhusu na kuwaleta watoto wao kujifunza soka.
Taratibu za kujiunga na kituo hicho zinapatikana siku ya uzinduzi kwa kushirikiana na serikali ya mtaa.
Ivo Mapunda ni miongoni mwa wachezaji wa Tanzania ambao wamecheza soka kwa mafanikio makubwa.
Comments
Post a Comment