MORINHO APIGWA "STOP" MCHEZO WA UNITED DHIDI YA SWANSEA JUMAPILI HII
Chama cha soka cha England FA November 2 kimetangaza kuwa Kocha Jose Mourinho amepigwa faini ya pauni 50,000 na kufungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi katika mechi moja.
Kocha huyo wa Man United amepigwa faini hiyo kufuatia kutoa maoni juu ya mwamuzi Anthony Taylor kabla ya mchezo wao dhidi ya Liverpool mwezi jana. Makocha huwa hawarusiwi kuwazungumzia waamuzi kabla ya mchezo.
Morinho amefungiwa kukaa kwenye benchi kwa mechi moja kufuatia kutoa maneno mabaya kwa mwamuzi Mark Clattenburg katika mchezo dhidi ya Burnley jumamosi iliyoisha, kifungo hicho atakitumikia mechi ya jumapili hii dhidi ya Swansea.
Comments
Post a Comment