WAMAREKANI KUAMUA MUSTAKABALI WA NCHI YAO
Baada ya kufanya mazoezi kwa kawaida kinachofuata ni mechi ili uamini kuwa mazoezi uliyofanya kweli yamekuwa na faida baada ya matokeo utajua kuwa mbivu na mbichi ziko wapi, lakini huwa zinakuwa mbaya kama mchezo wenyewe ni wa mtoano maana ukifungwa ndio basi hadi usubiri msimu unaofuata ujiandae upya.
Uchaguzi Mkuu nchini Marekani unafanyika Leo Novemba 8 na kila mmoja ana mtu wake anayemshabikia; uchaguzi wa Marekani ni uchaguzi wa dunia nzima sio wa taifa hilo pekee, hii inatokana na taifa hili kuwa na nguvu sana duniani na taifa ambalo kwa kawaida tunaweza kusema linaitawala dunia.
Msuguano mkali upo kati ya Chama cha Democratic pamoja na Republican, kwa upande wa Republican ambapo anakiongoza Donald Trump kulikuwa na watu wengi walikuwa katika mchuano hadi kuchaguliwa yeye wakati huku kwa Democratic walikuwa watiania watano na Clinton akiteuliwa kutetea chama hicho.
Kila mmoja anawasifu wake ikiwa Clinton aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje lakini pia Mke wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Bill Clinton huku Trump akiwa mfanyabiashara maarufu; swali ni kwamba nani atakayeibuka mshindi ? Swali gumu sana kwa kuwa kila mmoja alikuwa na mapugufu yake, Mchungaji maarufu wa Nigeria TB Joshua amesema kuwa Clinton ataibuka na ushindi katika uchaguzi huo je ni kweli ? Au ndio utabiri kila mmoja anaweza kusema hasa akiangalia aina na mchakato mzima unavyoenda. Acha tuone muda ukituambia ‘time will tell’ nani atavua mabua kati ya wawili hawa.

Comments
Post a Comment