TRUMP AMPIGA BAO CLINTON MAJIMBO MUHIMU MAREKANI
Trump anakadiriwa kushinda West Virginia, Kentucky, Indiana, Tennessee, South Carolina, Oklahoma na Alabama.
Clinton anakadiriwa kushinda Vermont, jimbo anamotoka Bernie Sanders, New Jersey, DC, Massachusetts, Maryland, Delaware, Illinois na Rhode IslandWapiga kura zaidi ya 45 milioni walipiga kura mapemaMuda wa kupiga kura eneo la Durham, North Carolina umeongezwaGeorge W Bush amesema hakupigia Clinton au Trump kura ya urais.
Wagombea urais wawili wakuu wa urais Marekani Hillary Clinton na Donald Trump wanakaribiana sana katika matokeo ya uchaguzi wa urais katika majimbo muhimu yanayoshindaniwa.
Clinton ameshinda Virginia naye Trump akashinda Ohio, Florida, na North Carolina.
Kwa sasa Trump ana kura 222 za wajumbe na Clinton 209. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.
Lakini mgombea wa Republican Bw Trump ameshinda majimbo mengi ya kusini mwa Marekani naye Bi Clinton akashinda majimbo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la utangazaji la ABC News.
Chama cha Republican kinaonekana kuwa njiani kuhifadhi wingi wa wabunge katika Bunge la Wawakilishi.
Kama ilivyotarajiwa, Bw Trump ameshinda katika ngome za Republican katika majimbo ya Alabama, Kentucky, South Carolina, Nebraska, Indiana, West Virginia, Mississippi, Tennessee, Oklahoma na Texas, ABC News wanakadiria.
Bw Trump pia anakadiriwa kushinda Arkansas, Kansas, North Dakota, South Dakota, Montana na Wyoming.
Shirika hilo linakadiria Bi Clinton atashinda ngome za Democratic majimbo ya New York, New Jersey, Connecticut, Massachusetts, Maryland, Vermont, Delaware, Illinois, Rhode Island na District of Columbia.
Mshindi anahitaji kupata kura 270 kati ya jumla ya kura 538 za wajumbe ndipo atangazwe mshindi.
Comments
Post a Comment