SIKU ZA ANTONY MARTIAL MANCHESTER UNITED ZINAHESABIKA
Jose Morinho amemuonya Anthony Martial anayecheza chini ya kuwango kuwa nafasi yake Manchester United inazidi kupotea.
Martia aliachwa kwenye kikosi kilichozuru Feyenoord katika mechi ya Ligi ya Uropa Alhamisi usiku, ambapo United walishinda 4-0, Henrikh Mkhitaryan akishinda kama mbadala wa nafasi ya Mfaransa huyo.
Kinda huyo wa miaka 20 akitokea Monaco alijiunga na Manchester United kwa dili ambalo lilidaiwa kufika hadi paundi milioni 58 na kujizolea umaarufu katika goli bomba alilofunga dhidi ya Liverpool katika mechi yake ya kwanza kati ya mabao yake 17 ya msimu uliopita.
Comments
Post a Comment