KOCHA STAND UTD ATAMBA KUISAMBARATISHA SIMBA SC

Tokeo la picha la stand united fc vs simba sc
Kocha wa Stand United Athuman Bilal ambaye ameachiwa timu na mfaransa Patrick Liewig, ameshakiongoza kikosi hicho katika mechi 5 akishinda mechi moja, sare tatu na kupoteza mechi moja.
Leo atakuwa kwenye mtihani mwingine katika kibarua chake atakaposimamia bechi la ufundi kuiongoza Stand United kuikabili Simba SC kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Bilal amesema hana hofu na Simba kwasababu tarari anarekodi ya kuwafunga na anawamudu vizuri huku akisisitiza kuwa, anajua namnaya kucheza na timu kubwa.
Tunaingia kwa ajili ya kuifunga Simba
“Tunaingia kwa ajili ya kushinda, Simba ni mpinzani wetu kwasababu hadi sasahivi bado hajafungwa sisi tumepoteza mchezo mmoja, tukiwafunga tunaendelea kubaki kwenye nafasi nzuri  na lengo letu ni kubaki katika nafasi za juu, kwahiyo Simba lazima afungwe.”
“Mwaka huu tumejipanga kiupinzani, Simba ninauwezo nayo nasubiri kuwastaajabisha watanzania. Sijaona ubora wa Simba wala ugumu wake uko wapi kwasababu wachezaji wengi ni walewale wa nchi hii wameongezeka wachache ambao walikuwa Mtibwa tayari tulisha kutana nao hawatakuwa wapya.”
Bilal kufuata nyayo za Liewig
Baada ya kuwafunga Yanga akiwa kama kocha msadizi chini ya Patrick Liewig, Bilal amesema baada ya kuondoka kwa mfaransa Liewig anataka kuonesha uwezo wake kwa kuifunga Simba kwasababu haitakuwa mara yake ya kwanza kuwafunga wakali hao wa Msimbazi.

Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YATAMBA KUENDELEZA REKODI YAO LEO

SINEMA YA CUF NA PROF LIPUMBA YAFIKIA PATAMU